Telegram ni moja kati ya mitandao maarufu ya mawasiliano inayotumiwa na watu wengi sana, hivi karibuni mtandao wa Telegram umefikisha watumiaji zaidi ya Milioni 500 kwa mwezi hii ikiwa inadaiwa kuwa ni ongezeko la asilimia 25 kulingana na mwaka jana 2020 kipindi cha mwezi wa pili.
Kukuwa huku kunachangiwa na mtandao huo kuwa na sehemu mbalimbali ambazo kwenye programu nyingine za mawasiliano hakuna. Moja ya sehemu hizo ni sehemu ya Bots ambayo inakupa uwezo wa kutumia programu hiyo zaidi.
Kupitia makala hii tutaenda kuangalia Telegram Bots mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufanya mambo mengi kwa urahisi na haraka. Kitu kizuri ni kuwa mtu yoyote anaweza kutumia bots hiz moja kwa moja kwenye app ya Telegram ya mfumo wowote.
Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja tuangalie bots hizi ambazo zitakusaidia kufanya mambo kwa urahisi kupitia Telegram.
TABLE OF CONTENTS
Telegram Bots
Kumbukua unaweza kutumia bots hizi kwa kufuata maelekezo ya bot husika mara baada ya kubofya kitufe cha Start kwenye bots husika ndani ya app ya Telegram.
YouTube Bot
Utubebot ni bots ambayo itakusaidia kudownload nyimbo mpya moja kwa moja kupitia app ya Telegram, kitu kizuri ni kuwa unaweza kupakua Audio na Video moja kwa moja kupitia app ya Telegram. Unaweza kusoma maelezo hapa kujua jinsi ya kutumia bot hii.
File Converter Bot
Kama unataka ku-convert mafile kwa haraka basi unaweza kutumia newfileconverterbot kuweza kufanya hivyo. Kupitia bot hii unaweza kubadilisha formati ya picha, video au hata audio kwenda kwenye format yoyote unayo pendelea
Tweet It Bot
Tweet It Bot ni aina nyingine ya bot ambayo itakusaidia kuweza kupost kwenye akaunti yako ya Twitter kupitia telegram, kupitia bot hii utaweza kupost picha, maandishi na hata video moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Twitter bila kutumia app au website ya Twitter.
Drop Mail
DropMailBot ni bot nyingine ya Telegram ambayo itakusaidia kuweza kutengeneza barua pepe za kutumia kwa muda mfupi. Kama kwa namna yoyote ulikuwa unataka barua pepe ya kutumia kwa muda mfupi basi bot hii itakusaidia sana, unaweza kutengeneza barua pepe moja kwa moja kupitia telegram.
Text to Speech Bot
Kama kwa namna yoyote unataka kubadilisha maneno ambayo unaongeza kutoka sauti kwenda kwenye maandishi basi bot hii itakusaidia sana. Kupitia bot hii unaweza kuongea na app ya telegram kisha bot hii itakupa maneno uliyoongea kupitia kwenye maandishi.
Hitimisho
Na hizo ndio baadhi ya bot ambazo unaweza kutumia kupitia Telegram na kuweza kufanya mambo mbalimbali, kumbuka kuwa hakikisha unakuwa na programu ya Telegram kwenye simu yako kabla ya kuanza kutumia bots hizi au kabla ya kubofya link kwa ajili ya kuwezesha bot husika.
Kumbuka pia wewe unaweza kutengeneza bot zako kupitia Telegram na unaweza kufanya hivyo kupitia hatua ambazo tutazionyesha kupitia channel yetu hapa. Kama bado huja subscribe nakushauri subscribe ili usipitwe na msimu mpya wa mafunzo kutoka Tanzania Tech.
Pia kama unataka habari moja kwa moja kupitia app ya telegram unaweza kujiunga nasi kupitia Channel yetu ya Telegram hapa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.