Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Vizuri Huduma ya Tigo Business

Fahamu Vizuri Huduma ya Tigo Business Fahamu Vizuri Huduma ya Tigo Business

Millcom ni kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ambayo makao makuu yake yanapatikana huko Luxembourg, Europe, kampuni hii inahudumia zaidi ya watu milioni 63 duniani kote kampuni hii hutoa huduma kupitia jina lake maharufu la Tigo na inatoa huduma kwenye nchi za Africa na Hispanic America.

Kampuni hii inayo ongezeka kukuwa kila siku ni moja kati ya kampuni zinazotoa huduma nafuu na salama kwa watumiaji wa simu Tanzania pamoja na nchi jirani, katika kutoa huduma hizo bora Tigo imeanzisha promosheni nyingi mbalimbali na maharufu ikiwa pamoja na ile ya kutumia WhatsApp bure kabisa na vifurushi maalumu vya wanafunzi wa chuo maarufu kama “University Offers”.

Advertisement

Tigo inaendelea kuongeza unafuu wa mawasiliano kwa kuleta huduma ya “Tigo Business” huduma hii imekuwepo kwa muda sasa lakini watu wengi hawaifahamu ndio maana leo Tanzania tech tunakuletea ufafanuzi wa huduma hizi kama ilivyoandikwa kwenye website ya Tigo Tanzania.

Tigo Business imegawanyika katika sehemu kuu mbili sehemu hizo ni kama zifuatazo:

  • Huduma za Simu
  • Internet

Huduma za Simu

Huduma hii itamsaidia mtumiaji wa Tigo kujiunga na huduma ya Postpaid ambapo mteja ataweza kulipia kutokana na matumizi yake, yani unatumia alafu unakuja kulipia mwisho wa mwezi au baada ya wiki kutokana na mkataba baina ya Tigo na mtumiaji.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii tembelea tovuti ya [button type=”default” text=”Tigo Tanzania” url=”http://www.tigo.co.tz/sw/business/mobile-solutions/mobile-solutions” open_new_tab=”true”] na upate habari zaidi.

Internet

Hii ni huduma nyingine inayopatikana katika Tigo Business ambayo inakupa huduma kemkem za internet ikiwa pamoja na huduma za APN kwa makampuni, mkonga wa mawasiliano, mawasiliano MPLS pamoja na Internet binafsi.

Soma zaidi kuhusu huduma ya [button type=”default” text=”Tigo Business” url=”http://www.tigo.co.tz/sw/business” open_new_tab=”true”] ili uweze kujua zaidi kuhusu huduma hii bora na makini inayoletwa na Millcom kwa kutumia Jina lake kubwa kabisa la Tigo.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use