Fahamu Vizuri Simu ya Samsung Galaxy Grand Prime Plus

Sasa ni wakati wa kumfahamu shujaa aliye rudi kutoka samsung
Samsung Galaxy Grand Prime Plus Samsung Galaxy Grand Prime Plus

Karibuni tena kwenye mapitio ya hapa Tanzania Tech, leo tunaenda kuangalia kwa undani simu mpya kutoka Samsung yaani Samsung Galaxy Grand Prime Plus, simu inayojulikana kwa slogan yake maarufu ya “shujaa karudi”. ikiwa ina maana simu hii ni toleo lingine la mfululizo wa simu ya Samsung Galaxy Grand Prime iliyotoka mwaka 2014, basi moja kwa moja bila kupoteza muda twende tukaanze uchambuzi huu.

  • Muundo wa Samsung Galaxy Grand Prime Plus

Katika swala zima la muundo Samsung imeamua kuleta simu ya gharama nafuu na yenye muundo wa kawaida ili kurahisishia kutumia, simu hii imetengenezwa kwa plastic ikiwa na vibonyezo vya sauti pamoja na kibonyezo cha kuwasha kwa upande wa kulia na kwa upande wa juu simu hii inasehemu ya kuchomeka earphone wakati kwa chini ina sehemu ya kuchomeka USB pamoja na chaji ukigeuza simu hii kwa mbele ina kibonyezo cha home pamoja na kibonyezo cha kurudi sambamba na kibonyezo cha menu. Tukigeuza kwa nyuma simu hii ina mfuniko wa plastic ambao unafunguka ili kukupa nafasi ya kuweka line, Memory Card pamoja na battery ili kuwasha simu yako.

Advertisement

  • Kioo cha Galaxy Grand Prime Plus

Baada ya kuwasha simu yako sasa twende tukaangalie kioo cha simu hii, Kioo cha simu hii ni tofauti na vioo vya AMOLED ambavyo Samsung hutumia kwenye simu zake za gharama kwani kioo cha simu hii kimetengenezwa kwa teknolojia ya qHD au TFT display kikiwa na ukubwa wa inch-5 sawa na pixel 540 x 960.

  • Processor na Memory

Kwa upande wa processor na memory ya simu hii inatumia RAM ya GB 1.5 pamoja na processor ya quad-core 1.4 GHz Cortex-A53 ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa Mediatek MT6737T,vile vile simu hii ina inatumia GPU ya Mali-T720MP2 ambayo inakupa uwezo wa kucheza game za kawaida pamoja na kutumia simu yako kwa mambo ya kawaida na kwa kasi inayotakiwa. Kwa upande wa memory ya ndani simu hii inayo memory yenye ukubwa wa GB 8 ikiwa ina kupa uwezo wa kuongeza ukubwa huo kwa kutumia memory card mpaka GB 256.

  • Internet na Muunganisho

Kwa upande wa internet pamoja na muunganisho simu hii inatumia line mbili ikiwa imewezeshwa na teknolojia ya kisasa ya 4G LTE pamoja na GPS yenye teknolojia ya Glonass, kwa upande wa Bluetooth simu hii inatumia Bluetooth ya toleo la 4.2 pamoja na Wi-Fi yenye speed ya 802.11 b/g/n. Vilevile simu hii inakuja na teknolojia ya NFC, Wi-Fi Direct, hotspot pamoja na uwezo wa kusikiliza redio za FM.

  • Kamera

Kwa upande wa kamera Samsung Galaxy Grand Prime Plus inakuja na kamera ya megapixel 8 kwa nyuma ikiwa na teknolojia ya autofocus, pamoja na flash ya LED. Kwa mbele simu hii ina kamera ya megapixel 5 yenye uwezo wa f/2.2 pamoja na flash ya LED kwa mbela. Pamoja na kuonekana kuwa na kamera ndogo bado simu hii inapiga picha vizuri na kuchukua video angavu za pixel 720 kwa kwa kasi ya 30fps (frame per second).

  • Mfumo wa uendeshaji

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji au Operation Syteam simu hii inatumia mfumo wa awali wa Android OS, toleo la 6.0 (Marshmallow) ikiwa ni toleo la kabla ya toleo la sasa la Android 7.0 Nougat.

  • Battery

Tukiamia upande wa battery simu hii inatumia battery ya kutoa yenye teknolojia ya Li-Ion pamoja na ukubwa wa 2600 mAh ikiwa na uwezo wa kukaa masaa 12 kama unaongea na simu na zaidi ya masaa 59 kama una sikiliza muziki pekee, simu hii inakaa na chaji karibia siku nzima kama utatumia simu hiyo kwa matumizi ya kawaida na hii ni pale tu utakapo chaji battery ya simu hii kwa dakika 175 sawa na masaa 2 na dakika 95 mpaka kujaa kabisa chaji asilimia 100.

  • Bei

Kwa upande wa bei simu hii ya Samsung Galaxy Grand Prime Plus inauzwa kwa kati ya shilingi za tanzania TZS 299,000 kama utainunua simu hiyo hapa Tanzania kupitia mtandao wa simu wa Tigo Tanzania.

Hitimisho

Kifupi kwa mujibu wa watu mbalimbali pamoja na kuitumia simu hii kwa muda, simu hii ni bora kama unataka simu ya bei rahisi na yenye ubora kwaajili ya kufanya mambo ya kawaida kama vile kupiga simu, kutumia mitandao yote bila wasiwasi, kupiga picha na mambo mengine ya kawaida. Lakini kama wewe unataka simu yenye uwezo wa kufanya zaidi ya hayo kama vile kucheza game kubwa pamoja na programu zinazotumia memory na GPU kubwa basi hakika simu hii itakua sio chaguo bora kwako kwa sasa.

Kutokana na hayo yote hapo juu je nini maoni yako kuhusu simu hii mpya ya Samsung Galaxy Grand Prime Plus..? Je unadhani ina staili nyota ngapi..? Toa maoni yako kwa kuipa idadi ya nyota hapo chini.

Basi mpaka hapo ndio mwisho wa mapitio haya kama unataka kujua kuhusu mapitio mengine kwa haraka unaweza kudownload app yetu ya Tanzania Tech kupitia Play Store na Tuna ahidi kukuleta habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Youtube kupata habari na mafunzo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

18 comments
  1. picha zake hazina mvuto. tatizo nin? hususani kamera ya nyuma hutoa picha zenye ukungu na nyeusi sio kama aina ya Samsung ninazozijua au hii niliyonayo ni fake. naomba majibu maana nilinunulia Tigo shop

  2. Kweli Kwa maana ya sifa inazo nyingi lakini program zake ziko kama za tecno ndo maana siipendi haiko kaMA SAMSUNG nyingine

  3. Maoni*simu zenu mbona mnauza. kwa bei ghali. sana ,mbona hazihimili. chaji

  4. ;simu yangu sumsung galaxy grand prime plus mbona ina tatizo la kamera ya nyuma inakua inaonyesha ukunguuu 2 haionyeshi picha vzuri na inaonyesha picha nyeusi….nini shida kwa hii au kamera yake ndivyo ilivyo. Na mtanisaidiaje…

  5. Ningependa kujua samsung galaxy grand prime plus inaingiza maji? İ mean ikitumbukia kwenye ndoo ya maji bado itaendelea kuwaka au ndio itazima

    1. Ni vizuri kuangalia sifa kamili za simu hii kama imethibitishwa kama haingii maji, vinginevyo weka simu yako mbali na maji.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use