Kabla ya kuanza ni vyema ujue kidogo kuhusu App hii na mtengenezaji wake. Kwa ambao mlikua hamjui App hii imetengezwa na Edward Snowden na kama jina hili ni geni kwako basi huyu alikuwa mfanyakazi wa CIA na alikuwa akifanya kazi za kompyuta kwenye serikali ya marekani.
Kwa wale ambao mmesha angalia filamu ya Snowden, nadhani mtakua mnajua kisa kizima cha Edward Snowden kuacha kazi kwenye kitengo cha CIA, lakini kama hujangalia basi chukua muda wako christmas hii kuangalia filamu hiyo utajua zaidi kuhusu huyu jamaa.
Sasa basi baada ya kusema hayo turudi kwenye teknolojia, hivi karibuni kitengo maalum kinachoitwa guardian project kinacho ongozwa na Edward Snowden kimetoa programu maalum ya Android inayoitwa Haven, Programu hii itakusaidia kuweka ulinzi sehemu unayokaa kwa kutumia simu yako ya Android.
Programu hiyo itakupa uwezo wa kuchukua sauti za watu, video, picha na hata mabadiliko ya mitetemeko na mwanga kwenye chumba chako yaani kama taa imezimwa au kuwaka, yote haya kwa kutumia simu yako ya Android.
Jinsi programu hiyo inavyofanya kazi ni kuwa, una download programu hiyo kwenye simu yako ya Android ambayo huitumii mara kwa mara, yaani ile ambayo hutembei nayo (mara nyingi unaiacha nyumbani) kisha una weka sehemu ambayo unataka ichukue picha, video au sauti kwenye nyumba yako kisha kila mara kutakapo kuwa na chochote kwenye nyumba yako simu hiyo itatuma data hizo moja kwa moja kwenye simu yako unayotumia.
Mbali ya hayo kwa mujibu wa tovuti ya Thenextweb, programu hiyo inahifadhi data hizo moja kwa moja kwenye simu hiyo na pia meseji unazotumiwa zinalindwa na mfumo wa end-to-end encryption maana yake ni kuwa hawezi kuzisoma mtu yoyote yule hata ambaye amefanya udukuzi kwenye simu yako.
Unaweza kujaribu programu hiyo ambayo kwa sasa iko kwenye hatua za majaribio kwa kubofya hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa Play Store kwaajili ya kupakua programu hiyo. Kujua zaidi kuhusu App hii unaweza kutembelea ukurasa maalum wa programu hiyo Hapa.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.