Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Njia Rahisi ya Kukuza Akaunti yako ya Instagram

Kuza akaunti yako ya Instagram kwa kutengeneza muonekano wa kipekee
Fahamu Njia Rahisi ya Kukuza Akaunti yako ya Instagram Fahamu Njia Rahisi ya Kukuza Akaunti yako ya Instagram

Ni wazi kuwa Instagram ni sehemu ya muhimu sana hasa kwa mtu anaefanya biashara hapa Tanzania, hii inatokana na kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanatumia Instagram kuliko mitandao mingine ya kijamii.

Kuliona hilo leo nimekuletea njia mpya ambayo inaweza kukusaidia sana kukuza akaunti yako ya Instagram kwa urahisi na haraka.

Advertisement

Ni wazi kuwa kunazo akaunti nyingi sana kwenye mtandao wa Instagram hivyo ni muhimu sana kuwa na muonekano bora kwenye akaunti yako, muonekano ambao utakusaidia kuvutia wateja wengi kwa haraka na urahisi.

Baada ya kusema hayo sasa ningependa ufahamu njia hii rahisi, Kupitia soko la Play Store au App Store unaweza kupakua app inayoitwa FocoDesign. Unaweza kupata app hii kupitia link hapa kwa android au kupitia hapa kwa iOS, pia unaweza kudownload kupitia hapo chini.

App hii inakupa uwezo wa kisasa na wa kipekee wa kuweza kuedit picha zako kwa ajili ya mtandao wa Instagram. Kupitia app hii unaweza kutumia Templent mbalimbali ambazo zitafanya akaunti yako ya Instagram kuwa ya kipekee na kuvutia wateja zaidi.

App hii ni rahisi sana kutumia na mtu yoyote anaweza kutumia hivyo sitopoteza muda mwingi wa kukufundisha jinsi ya kutumia. Baada ya kupakua app hii unaweza moja kwa moja ukaendelea kwa kuchagua mtindo unao utaka na moja kwa moja utaweza kutengeneza muonekano wa tofauti wa akaunti yako ya Instagram.

Kama unataka kujifunza zaidi njia ya kukuza akaunti yako ya Instagram unaweza kuangalia video hapo chini kujua jinsi ya kupata likes nyingi kwenye akaunti yako ya Instagram, pia unaweza kusoma zaidi hapa.

Pia unaweza kujifunza njia mbalimbali za kutumia akaunti yako ya Instagram kisasa kabisa kwa kuangalia video hapo chini. Au unaweza kusoma zaidi hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use