Ni wazi kuwa kila mtu anajua kuwa kumiliki channel kwenye mtandao wa YouTube ni moja kati ya biashara zinazofanywa na vijana wengi wa kitanzania.
Lakini kumekuwa na mawazo ya tofauti sana kuhusu kiasi cha pesa channel au video inachotengeneza kupitia mtandao huo. Ni watu wachache sana hapa Tanzania ambao wako tayari kuonyesha data za akaunti zao na kuweza kuonyesha ni kiasi gani ambacho channel zao zinatengeneza kwenye mtandao wa YouTube.
Inawezekana wewe ni mmoja wa watu mbao wanafikiria kumiliki channel kwenye mtandao wa YouTube na unataka uweze kushawishika kwa kujua ni kiasi gani ambacho kimetengezwa na channel au video ambazo pengine unazitizamia kama moja ya inspiration zako.
Kuliona hili nimekuletea njia rahisi ya kuweza kujua ni kiasi gani ambacho channel inaweza kutengeneza kulingana na idadi ya views ambazo imepata.
Kumbuka ni muhimu kujua kuwa kiasi kinacho onekana kutokana na makadirio, kumbuka kiasi hicho kinaweza kuzidi au kupungua kutokana na mahali video zilipo angaliwa, ikiwa pamoja na mambo mengine.
Kwa kuanza unatakiwa kujua CPM na CPC, unaweza kusoma makala yetu iliyopita kujua zaidi kuhusu CPC na CPM.
Lakini makala hii itaenda kuangalia CPM ya Afrika Mashariki ambayo hii mara nyingi ni 1.00. Kumbuka inaweza kuzidi au kupungua.
Baada ya hapo tembelea Link hapo chini kisha utapelekwa kwenye tovuti ambayo inaweza kukusaidia kuweza kujua video au channel inalipwa kiasi gani cha pesa kutokana na views.
Kupitia sehemu ya view iliyopo juu kushoto andika idadi ya view kwa mfano 10000 sawa na view elfu kumi. Sehemu ya pili ambayo inakuwa na namba 4.00 badilisha na andika 1.00.
Baada ya hapo bofya sehemu ya Calculator na utaweza kuona kiasi ambacho kwa makadirio ya channel au video imetengeneza.
MUHIMU : Hakikisha una angalia namba ya kwanza ambayo ni “Estimated Daily Earnings” hapa ndio utaweza kuona kuwa kwa mfano kwa hapa Tanzania video ikifikisha views 10,000 na imeangaliwa na watanzania au watu wa africa mashariki inaweza kutengeneza kati ya dollar $2.50 hadi $10.
Kiasi hicho kinaweza kisiwe kama ilivyo kwa asilimia 100% lakini kiasi hicho ni lazima kitakuwa kati ya dollar $2.50 hadi $10.00 kwa views hizo 10,000.
Kwa view (laki moja) 100,000 au 100k video ikiangaliwa na watu Afrika Mashariki unaweza kutengeneza kati ya dollar $25 hadi $100.
Kwa views milioni moja 1,000,000 au 1M video inaweza kutengeneza kati ya dollar $250 hadi $1000. Kumbuka hayo ni makadirio tu pesa hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na mahali watu walipoangalia video zako. Lakini baada ya kupata views Milioni 1 ni lazima kiasi kitakua kati ya $250 hadi $1000.
Kama unataka kujua kiasi cha pesa ambacho channel nzima imetengeneza kwa muda wote unaweza kuangalia kwenye sehemu ya about ya kwenye YouTube channel yoyote.
Kwa mfano ukitaka kuangalia channel ya millard Ayo imetengeneza shilingi ngapi hadi sasa unaweza kuchukua namba ya views kwenye channel yake kupitia sehemu ya about. Kwa sasa channel hii ina jumla ya views 1,631,161,638.
Kama unavyoweza kuona channel hii hadi sasa imetengeneza kati ya dollar $400,000 hadi dollar $1,000,000. Kiasi hichi kinaweza kuongeneza au kupunguka.
Kwa kutumia njia hii na uhakika utaweza kujua kiasi cha pesa ambacho channel yako au channel yoyote inaweza kutengeneza au video. Na uhakikia hii inaweza kuwa inspiration kwako kuanzisha channel kupitia mtandao wa YouTube.
Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia pakua app ya Tanzania Tech ili kupata kujifunza kwa haraka zaidi.