Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Utaweza kupata ujumbe mfupi wa kuonyesha mtu anapokuwa online au offline
Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Ni wazi kuwa Internet imekuwa ni sehemu ya muhimu sana kwenye maisha yetu, lakini pia ni wazi kuwa mitandao imekuwa ni sehemu kubwa ya kuharibu watoto wetu hasa wanapokuwa wakitumia mitandao hiyo kwa njia ambayo sio sahihi.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kupata taarifa pale mtu anapokuwa online na ni muda gani ambao ametumia kuwepo online. Njia hii itakusaidia sana wewe kama mzazi kuweza kuthibiti tabia za watoto wako na kujua ni muda gani wanatumia kuchati kwenye programu hiyo.

Advertisement

Kumbuka ni muhimu kutumia njia hii kwa usahihi na usitumie njia hii vibaya kwa namna yoyote, makala hii ni kwaajili ya elimu na hatuta husika kwa namna yoyote jinsi utakavyo tumia njia hii. Kwa kusoma makala hii unakubali vigezo na masharti.

Pia kumbuka kuwa njia hii sio udukuaji bali hii ni huduma ambazo zina tolewa na apps mbalimbali ambazo zinapatikana kwenye soko la Play Store na App Store.

Kwa kusema hayo moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kudownload app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload app hiyo moja kwa moja endelea kwa kusoma maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii, fungua app hii kisha utapelekwa kwenye ukurasa wa kwanza ambayo unatakiwa kufanya setup zifuatazo.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Hatua ya ili bofya kwenye kitufe cha mtu chenye jumlisha kinacho patikana juu upande wa kulia.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Baada ya kubofya sehemu hii moja kwa moja itafunguka sehemu nyingine ambayo unatakiwa kuweka namba ya mtu au mtoto ambaye unataka kupata Notification anapokuwa online. Andika jina lolote kwenye sehemu ya jina.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Sehemu ya Country Code, bofya hapo na tafuta jina la nchi uliyopo. Kama upo Tanzania basi hakikisha sehemu hii ina anza na +255, pia kama upo Kenya hakikisha sehemu hiyo ina anzia na +254. Kwa urahisi unaweza kutumia sehemu ya kusearch kupata jina la nchi yako kwa haraka.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Baada ya hapo sehemu ya Phone Number andika namba ya simu iliyopo kwenye WhatsApp ambayo unataka kupata Notification au taarifa pale mtu huyo au mtoto anapokuwa online. Hakikisha huanzi na sifuri bali anza kuandika namba bila kuandika sifuri.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Baada ya kumaliza hatua zote hizi sasa malizia kwa kubofya kitufe cha TRACK, ambacho kipo chini kabisa ya ukurasa huo. Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambao utakuonyesha namba na kama namba hiyo ipo online au lah.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Hatua ya mwisho ya muhimu ni kuwasha sehemu ya Notification au taarifa, unachotakiwa kufanya ni kubofya kitufe cha settings kwenye ukurasa huo hapo juu. Kisha washa sehemu za Notification kwenye namba husika.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Kama unataka kupata taarifa kama yuko offline au muda ambao kaacha kutumia programu ya WhatsApp basi unaweza kuwasha pia sehemu ya Offline Notifications. Baada ya hapo sasa unaweza kufunga programu hiyo na mara mtu huyo anapokuwa online au offline utaletewa ujumbe.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Pia unaweza kuingia ndani ya app hii na utaweza kuona Alama ya njano na muda ambao mtu huyo au mtoto wako yupo Online. Pia utaletewa taarifa baada ya mtu huyo kutoka kwenye WhatsApp na ni muda gani ambao ametumia kwenye programu ya WhatsApp.

Pata Ujumbe Mfupi Mtu Anapokuwa Online WhatsApp

Kwa kufuata njia hizi moja kwa moja utakuwa umeweza kujua ni muda gani mtu anapokuwa online kwenye programu ya WhatsApp na muda gani anakuwa offline na ni muda gani anatumia kwenye programu hiyo. Pia programu hii inafanya kazi hata kama mtu amezima sehemu ya last seen na haitaji kuwa na namba ya mtu huyo kwenye simu yako.

Bila shaka njia hii utaitumia kuweza kufanya matumizi ya mtandao kuwa bora kwa watoto wako, kama unataka kujua njia zaidi za kulinda watoto wako na mtandao, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza akaunti ya mtoto ya Google moja kwa moja na kuweza kuzuia programu ambazo anaweza kutumia. Kwa maujanja zaidi subscribe kwenye channel yetu hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use