Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Yazindua Huduma ya Bots on Messenger

Facebook Yazindua Huduma ya Bots on Messenger Facebook Yazindua Huduma ya Bots on Messenger

Facebook imetangaza rasmi kuzindua huduma ya Bots on Messenger kwenye programu yake ya Facebook Messenger kwa wale tusiojua “Bots on Messenger” ni aina ya roboti ambazo hizi utengenezwa maalumu kujibu meseji mbalimbali pale unapokua unachat, kwa mfano labda unataka kujua hoteli nzuri ya kulala ilipo unaweza kuuliza hizo “Bots on Messenger” kwenye programu ya Facebook messenger na hizo zitakusaidi kukupa majina ya hoteli maarufu za sehemu ulipo, Kama mfumo wa programu kama ya Telegram.

Mwenyekiti wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg alizindua huduma hiyo jana kwenye mkutano na wabunifu uliopewa jina la Facebook F8 akiwa kwenye mkutano huo Zuckerberg alisema programu hiyo iliyopewa jina la “bots on Messenger” itasaidia wafanya biashara mbalimbali kutoa huduma kwa wateja wao kirahisi zaidi kwa kujibu maswali ya wateja wao moja kwa moja kwa kutumia Facebook Messenger kupitia huduma hiyo mpya ya bots on messenger. Hata hivyo mkutano huo wa F8 bado unaendelea na ulipangwa kufanyika kwa siku mbili yani siku ya jana tarehe 12 na siku leo yani tarehe 13.

Advertisement

Tutawaletea habari zitakazoendelea kutufikia ikiwa pamoja na video ya tamasha hilo linalo fanyika huko marekani endelea kutembelea blog ya tanzania tech.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use