Wakati huu ambapo nchi nyingi watu wengi wapo nyumbani ni wazi kuwa sekta ya game imekuwa ni kimbilio la watu wengi kutokana na uwezo wake wa kufurahisha na kupoteza muda kwa haraka. Kuliona hili, kampuni ya Facebook hapo jana tarehe 20 mwezi Aprili imetangaza ujio wa App yake mpya ya Facebook Gaming.
Kupitia app hiyo watumiaji wata weza kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kucheza game mbalimbali za mtandaoni ambazo zipo ndani ya App hiyo, ku-stream na kuangalia game ambazo watu wanacheza pamoja na kuchat moja kwa moja ndani ya App hiyo.
App hii inafanana kabisa na mtandao wa Twitch ambao pia unaruhusu watumiaji wake kutazama pamoja na ku-stream game moja kwa moja wakiwa wanacheza game hizo Live. Mbali na Twitch, App hii pia imekuja kama mshindani wa sehemu ya YouTube Gaming, sehemu ambayo nayo pia inakuja na sehemu kama hizi za kuruhusu watu mbalimbali kuangalia na ku-stream game mubashara.
Kwa sasa ndani ya App hii unaweza ku-Follow watu mbalimbali ambao ni wapenzi wa game, ambapo pale wanapokuwa wanaonyesha game zao mubashara basi utaweza kuona kwenye sehemu ya mwanzo wa app hiyo unapofungua. Pia pembeni chini ya ukurasa huo, utaweza kuona sehemu yenye alama ya jicho ambapo hapo ndio patakupa uwezo wa kwenda (Live) mubashara na kuonyesha game zako jinsi unavyo cheza.
Ukurasa wa pili kutoka kushoto, utakupa uwezo wa kucheza game mbalimbali za mtandaoni ikiwa pamoja na kuonyesha baadhi ya watu walio cheza game hizo. Ukurasa wa tatu kutoka kushoto, hapo utaweza kuona game mubashara kutoka kwa wachezaji mbalimbali duniani, pia utaweza kufuata (follow) game mbalimbali ili ziweze kutokea kwenye ukurasa wako wa home pale mtu anapocheza game hiyo, pia utaweza kuona game hizo watu wakiwa wanacheza mubashara.
Ukurasa wa mwisho kutoka kushoto utaweza kukupa nafasi ya kuchati na watu mbalimbali ambao wamecheza baadhi ya game kupitia mtandao wa Facebook, hapo unaweza kumtumia mtu game pamoja na kufanya mambo mengine mbalimbali.
Kwa sasa tayari App hii inapatikana Play Store kwa watumiaji wa simu za Android, hivyo unaweza kujaribu app hii kwenye simu yako kwa kutumia link hapo chini. Kama link hiyo haifanyi kazi kwenye simu yako unaweza kupakua Facebook gaming kupitia hapa.
Kwa watumiaji wa vifaa vya iOS kwa sasa bado App hii haijafika kwenye soko la App Store ila endelea kutembelea ukurasa huu tutaenda kuongeza app hiyo pindi itakapo zinduliwa rasmi.