Facebook sasa yaitoa application yake ya “Live stream” kwa watumiaji wake wote, kwa wale wasio jua application hiyo ni kwa sababu application hiyo ilikua pekee kwa Mastaa wakubwa wa nchini marekani. Lakini kwa sasa application hiyo imeachiwa rasmi na facebook kuja kwa watumiaji wake wote dunia nzima, imeripotiwa baadhi ya video kutoka south Africa, Brazil, UK na ujerumani.
Update hizo zitamfanya mtumiaji wa facebook kushare video na dunia nzima pale anapokua akichukua live, nikama vile “live tv show”.
Ili kuangalia kama umepata update hiyo kwenye simu yako fuata maelekezo haya
Fungua applicaton yako ya facebook kisha chagua update status iliyoko juu karibia na option ilioandikwa “News feed” kisha bonyeza “new Live Video icon” itakuonyesha tangazo kwamba inapatikana kwenye simu yako. Kama umepata update hizo utakua na uwezo wa kuchangua ni nani unataka kushare nae video yako kisha utaweka utambulisho maalumu yani “Description” kisha utaanza kushare na wale ulio wachagua.
Facebook inatarajia kutoa update zake mpya za application yao kwenye iOS ndani ya wiki mbili zijazo. Kuhusiana na android facebook haijasema itatoa lini update zake ili kuwezesha Live Stream.