Facebook Yanunua Mtandao wa Giphy kwa TZS Bilioni 926

Kampuni ya facebook yazidi kuongeza ukubwa wa mtandao wake zaidi
Facebook Yanunua Mtandao wa Giphy kwa TZS Bilioni 926 Facebook Yanunua Mtandao wa Giphy kwa TZS Bilioni 926

Kampuni ya Facebook hivi karibuni imetangaza kununua mtandao wa Giphy kwa dollar za marekani milioni $400, sawa na takribani zaidi ya bilioni 900 za kitanzania. Giphy ni mtandao wa kijamii ambao unajulikana kwa kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wanaoshiriki picha au video fupi ambazo hazina sauti maarufu kama GIF.

Facebook Yanunua Mtandao wa Giphy kwa TZS Bilioni 926

Advertisement

Kwa mujibu wa Facebook, mtandao wa Giphy utaendelea kufanya kazi kama kawaidia bila mabadiliko yoyote kwa sasa, lakini facebook inategemea kuongeza watumiaji kwenye mtandao huo kwa kuunganisha mtandao huo moja kwa moja na mtandao wa instagram ambao tayari unayo sehemu ya kushiriki picha hizo zinazotembeea maarufu kama GIF.

Facebook Yanunua Mtandao wa Giphy kwa TZS Bilioni 926

“Watumiaji wanaweza kuendelea kuweka picha zao zinazo tembea kupitia mtandao wa Giphy bila kuwa na mabadiliko yoyote hadi hapo kampuni hiyo itakapo tangaza kufanya mabadiliko”, ilisema sehemu ya taarifa kutoka mtandao wa Facebook.

Hata hivyo inasemekana kuwa inawezekana kuwa facebook imetoa pesa nyingi zaidi kutokana na kuwa kiwango kilichotajwa hapo juu ni makadirio na sio kiwango ambacho facebook yenyewe imethibitisha. Kwa mujibu wa mtandao wa tovuti ya Reuters, inasemekana kuwa facebook ilikataa kutaja kiwango cha pesa ambacho ili lipa kununua mtandao huo.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka kujua kuhusu mtandao huo wa Giphy, unaweza kupakua app yake kupitia Play Store au unaweza kutembelea tovuti ya Giphy.com ili kutengeneza akaunti.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use