Hivi karibuni mtandao wa facebook umeripotiwa kuanza kufanya majaribio ya kufungua akaunti ya Facebook iliyofungwa kwa kutumia uso au (facial recognition).
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali sehemu hiyo itakuwa inafanya kazi kama akaunti yako imefungwa kutokana na sababu mbalimbali za kiulinzi na itakuwa ni moja kati ya sehemu ambazo zipo sasa kama zile za kumtambua rafiki yako wa karibu na ile ya kutumia ujumbe mfupi.
Hata hivyo facebook imeongeza sehemu hiyo kutokana na sehemu zilipo awali kutokufanya kazi kwa asilimia 100, huku baadhi ya watu wakishdwa kutambua majina ya marafiki kwenye mtandao huo ikiwa ni moja ya njia ambazo facebook huzitumia kuweza kufungua akaunti yako pale inapo fungwa kutokana na sababu za kiulinzi.
Kwa mujibu wa tweet ya muandishi wa habari za teknolojia kutokea tovuti ya The Next Web Matt Navarra, sehemu hiyo itaonekana kama hivyo na itakuwa ikifanya kazi kwenye vifaa vyenye kamera na inategemewa kufanyia utafiti mkubwa kabla ya kuzinduliwa rasmi.
NEW! Facebook working on a facial recognition feature to help secure your account
h/t Devesh Logendran pic.twitter.com/demol4dKj1
— Matt Navarra ⭐️ (@MattNavarra) September 29, 2017
Bado haija julikana lini sehemu hiyo itakuwa tayari lakini, kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.
Chanzo : Engadget
Maoni*endelen kutupatia habar kuhusu mabadiliko ya kimutandao
Asanten Mungu awabariki
Maoni*duh