Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Inakuja na Mtandao wa Kuuza na Kununua

Leo Facebook imetangaza rasmi kuwa itazindua mtandao wake wa kuuza na kununua mapema wiki hii
facebook-yaleta-mtandao-wa-kuuza-na-kununua facebook-yaleta-mtandao-wa-kuuza-na-kununua

Hivi karibuni kampuni ya Facebook kupitia tovuti yake ya Facebook ilitangaza rasmi kuwa sasa iko tayari kuzindua mtandao wake ambao utawasaidia watumiaji wake kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kupitia tovuti yake ya Facebook.

Facebook ambayo kwa sasa inayo zaidi ya watumiaji  bilioni 1.71 kwa mwezi imepanga kurahisisha huduma hizo za kuuza pamoja na kununua bidhaa mbalimbali ili kuwapa urahisi watu ambao kwa sasa hutumia magroup mbalimbali ya kuuza ama kununua ili kupata huduma hizo kupitia mtandao wake wa huo wa Facebook. Kukiwa na watu zaidi ya milioni 450 ambao hutembelea magroup hayo ya kuuza na kununua kila mwezi facebook imepanga kuleta huduma hiyo mapema mwanzoni mwa mwezi huu ili kuwezesha watu hao kuweza kuuza au kununua bidhaa kwa haraka na kwa urahisi. Hata hivyo Facebook imepanga kuanza kutoa huduma hizo mapema wiki hii kwa nchi za Marekani, Uingereza, Australia pamoja na New Zealand na baadae kwenye nchi zingine.

Advertisement

Kuhusu jinsi ya kutumia mtandao huo mpya Facebook imepanga kuleta sehemu mpya ambapo ndipo kitakuwa kinaonekana kitufe maalum ambacho mtumiaji anapo bofya kitufe hicho huletewa bidhaa mbalimbali ambazo facebook inahisi unahitaji (hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa ulizokua unaperuzi kwenye mtandao huo). Pia kama wewe unataka kuuza bidhaa zako kutakua na sehemu maalum ambayo itakuwezesha kuuza bidhaa zako kwa urahisi kabisa, huduma hiyo inatarajiwa kuja pia kwenye programu zote za mtandao huo za iOS pamoja na Android.

Facebook haijatangaza kama itakua ikitoza fedha kutumia huduma hiyo mpya hivyo kwa habari zaidi kuhusu huduma hiyo mpya kutoka Facebook endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use