Kampuni ya Facebook hivi leo imetangaza ujio wa programu yake mpya ya Facebook Messenger ambayo itakuwa ni kwaajili ya watumiaji wa kompyuta. Kwa sasa tayari programu hiyo mpya Messenger inapatikana kwa watumiaji wote wa mifumo yote ya macOS pamoja na Windows.
Kupitia programu hiyo mpya ya Facebook Messenger kwa ajili ya kompyuta, utaweza kufanya mambo yote ambayo unaweza kufanya kwenye programu yako ya Messenger kupitia simu yako. Hii ni pamoja na kupiga simu za video pamoja na kutumia muonekano wa giza au (Dark Mode) ambao utasaidia kulinda macho yako hasa wakati wa usiku.
Facebook imeahidi kuleta sehemu nyingine mpya zaidi kwajili ya programu hiyo, huku ikiwataka watumiaji wa mtandao wa Facebook kutumia zaidi programu hiyo hasa kipindi hicho ambacho watu wengi wanafanyia kazi nyumbani ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona au COVID-19. Kwa sasa kama unataka kujaribu programu hizo mpya unaweza kupakua programu hizo kupitia link hapo chini na utapelekwa kwenye masoko maalumu kulingana na mfumo unao tumia.
Facebook Messenger For Windows
Facebook Messenger For macOS
Mbali na Facebook Messenger, kwa sasa pia unaweza kujaribu muonekano mpya wa tovuti ya facebook.com muonekano ambao pia ni maalum kwa watumiaji wa kompyuta. Kujua jinsi ya kujaribu muonekano huo unaweza kusoma zaidi hapa.