Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Kutumia (AI) Artificial Intelligence Kupambana na Ugaidi

Facebook kuleta aina mpya ya kuzuia magaidi kutumia mtandao wake
facebook kupambana na magaidi facebook kupambana na magaidi

Katika kuongeza jitihada za kumbana na ugaidi duniani, kampuni ya Facebook imetangaza kuwa sasa italeta mfumo mpya wa AI au Artificial Intelligence ili kuzuia magaidi kutumia mtandao wake wa kijamii yaani Facebook.

Katika makala iliyo andikwa kwenye ukurasa wa habari wa mtandao huo, facebook imesema kuwa mfumo huo mpya utawezesha kuondoa post za magaidi kwa haraka kabla watu hawaja ziona post hizo. Hata hivyo katika ripoti iliyotolewa na mtandao wa skynews leo ilithibitisha kuwa sehemu hiyo ni kama ili inayotumika kuondoa picha za utupu za kwenye mtandao huo wa kijamii.

Advertisement

Katika taarifa hiyo facebook iliendelea kuandika kuwa kwa sasa inafanyia kazi mfumo mpya wa “text-based signals” ambao utafanya kazi ya kusoma baadhi ya post ambazo tayari zilisha ondolewa ili baadae mfumo huo kujifunza kuondoa post zinazofanana na hizo zinazo tumwa kwenye mtandao huo.

Hata hivyo facebook imeamua kwenda mbali zaidi na kuajiri zaidi ya watu 150 ambao kati ya hao ni maafisa usalama wastaafu, mawakili wastaafu pamoja na maengineer wapya wote hao wakiwa na lengo moja la kuzuia ugaidi kwenye mtandao wa facebook. Makala hiyo ilielezea kuwa yote hayo yamefanyika baada ya ugaidi uliofanyika hivi karibuni kupelekea watu kuuliza je makampuni ya teknolojia zaidi mitandao ya kijamii inasaidia vipi kuzuia ugaidi, na hilo ndio jibu lilio tolewa na Facebook kupitia Post Hii, unaweza kuisoma zaidi hapo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use