Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hii Ndio Njia Ambayo Facebook Inatumia Kujua Kuhusu Wewe

Hii ndio moja kati ya njia ambazo facebook hutumia kujua kuhusu wewe
facebook data facebook data

Facebook ni moja kati ya mtandao mkubwa sana wa kijamii, ukubwa wa mtandao huo umepelekea pia facebook kuwa moja kati ya mtandao ambao unaongoza kwa kukusanya data za watumiaji wake kuliko mtandao mwingine wa kijamii, ili kuweza kubaini hilo leo Tanzania Tech tunakuletea njia moja wapo ambayo facebook hutumia kukusanya data za watumiaji wake.

Njia hii imegunduliwa na kutengenezwa na kampuni ya ubunifu ya Data x kwa kushirikiana na chuo cha Cambridge pamoja na kampuni ya IBM ili kukujuza jinsi gani Facebook inavyokusanya data zako pale unapotumia mtandao huo. Wote tunajua kuwa wakati unataka kujisajili na mtandao huo unaulizwa jina namba za simu pengine kuna wakati unaulizwa hata ndugu zako, mpenzi au hata rafiki wa karibu, yote haya bila kujua hutumiaka kutengeneza profile yako ambapo facebook hutumia algorithm maalum kutafsiri data hizo na kujua kuhusu wewe zaidi ya unavyofikiria, unataka kujua zaidi endelea kusoma hapo chini..

Advertisement

Kwa kuanza hakikisha unatumia browser ya Google chrome kwenye kompyuta yako kwani njia hii inaweza kufanywa pekee kwenye kompyuta hivyo kama unataka kufuatilia hatua hizi hakikisha unatumia kompyuta na unatumia browser ya google chrome kisha fuata hatua hizi. Washa browser yako ya google chrome kama bado hujafanya hivyo kisha download na install kiunganishi (addon) cha Data Selfie kwenye browser yako, baada ya kuinstall ingia kwenye ukurasa wa facebook kisha endelea kutumia mtandao huo kwa muda kama dakika 10 mpaka dakika 20.

Wakati unatumia mtandao huo utaona kuna kiduara upande wa kushoto chini kikiwa kinahesabu namba, hapo inaonyesha programu hiyo inafanya kazi. Endelea kutumia mpaka dakika 10 au 20 zipite kisha bofya alama ya jicho iliyoko juu upande wa kulia alafu bofya Your Data Selfie hapo utaweza kupelekwa kwenye chati yenye kuonyesha ni muda gani umetumia facebook, post zipi umezipenda, link zipi umefungua pamoja na mambo mengine mengi. Unaweza kuhifadhi data zako kwenye kompyuta yako kwa kuzidownload kupitia kitufe cha Export Your Data, pia unaweza kuzifuta data zako moja kwa moja kupitia sehemu ya Delete Your Data. Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya Data X kifaa hichi ni salama kutumia na hakiifadhi data zozote kwenye server hivyo usiogope kuhusu kuibiwa data zako. Ukitumia Programu hiyo kwa muda mrefu inauwezo hata wa kukwambia unaonekanaje jaribu kutumia kama wiki hivi kisha tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kama unataka habari zaidi kuhusu teknoloja endelea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kupakua App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa wakati, pia unaweza kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube kama unataka kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use