Mwezi julai instagram ambayo ni sehemu ya kampuni ya Facebook ilianza kufanya majaribio ya kuficha idadi ya like kwenye picha mbalimbali kwenye mtandao wa Instagram. Majaribio hayo hadi sasa bado yanaendelea na inasemekana kuwa sehemu hii imeonekana kupendwa na watumiaji wengi kadri siku zinapokwenda.
Hiyo ni moja kati ya sababu iliyo sababisha Facebook nayo kuanza kufanya majaribio ya kuficha idadi ya Likes kwenye post mbalimbali ndani ya mtandao huo. Kwa mujibu wa tovuti ya Techcrunch ambayo imechapisha habari hiyo kutoka kwa mvujishaji maarufu mtandaoni Wong Mjane, sehemu hiyo itakuwa inafanya kazi kama ilivyo kwenye instagram huku ikiruhusu mwenye post mwenyewe pekee kuwa na uwezo wa kuona idadi ya like tofauti na sasa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Techcrunch, inasemekana kuwa Facebook ime thibitisha kuwa inategemea kuanza kufanya majaribio hayo hivi karibuni bila kutaja tarehe halisi ya kuanza kwa majaribio hayo. Hata hivyo inasemekana kuwa reaction pamoja na idadi ya comment au maoni ndio namba pekee itakayo kuwa inaonekana mara baada ya Facebook kuanza majaribio hayo ya kuondoa likes kwenye picha ndani ya mtandao huo.
Kwa sasa sehemu kama hii inaendelea kufanyiwa majaribio kwenye mtandao wa Instagram na inapatikana kwa watumiaji waliochaguliwa kutoka nchi mbalimbali. Kupitia sehemu hiyo watu wote hawatoweza kuona idadi ya likes kwenye picha husika isipokuwa mwenye picha mwenyewe.
Kujua zaidi kuhusu sehemu hii pale itakapo kuja hapa Tanzania, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kupakua app yetu ya Tanzania Tech kupitia mfumo wa Android.