Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Inakuja na Sehemu Mpya ya Downvote Kwenye Maoni

Sasa facebook kuruhusu kuonyesha ishara ya Downvote kwenye maoni
sehemu ya facebook Downvote sehemu ya facebook Downvote

Hivi karibuni mtandao wa facebook umeanza kufanya majaribio ya kuongeza sehemu mpya kwenye sehemu ya maoni (comment) ndani ya mtandao huo, sehemu hiyo mpya itawaruhusu watumiaji kuweza kuonyesha (downvote) kwenye maoni ambayo yamekiuka vigezo na masharti ya utumiaji wa mtandao huo.

Sehemu hiyo iliyopewa jina la downvote, itakuwa sambamba na sehemu ya Like ambayo hutumiwa kuonyesha ishara ya kupenda picha au maoni ndani ya mtandao wa Facebook.

Advertisement

Habari kupitia kwenye tovuti ya techcruch zinasema, sehemu hiyo ya downvote kwa sasa inafanyiwa majaribio na endepo ikifanikiwa kuwafikia watumiaji wote, itakuwa ni kwaajili ya kuzuia watumiaji wa mtandao huo kutoa maoni ambayo hayatakiwi au yanayo kiuka vigezo na masharti ya utumiaji wa mtandao huo wa Facebook.

Hata hivyo sehemu hiyo itakuja na sehemu zingine za kuchagua ambazo zitakuwa zikimtaka mtumia aliyebofya sehemu hiyo ya Downvote kuchagua ni kwanini anadhani comment hiyo au maoni hayo yaondolewe kwenye kurasa au picha hiyo. Kwa sasa sehemu hii inafanyiwa majaribio kupitia watu wachache huko nchini marekani na bado Facebook haijatoa ripoti ni lini sehemu hii inaweza kuja kwenye mtandao wa Facebook.

2 comments
  1. Nashukuru sana kwa habari za teknolojia ambazo m’nazidi kunitumiya. Na waomba sana tena san muendelee ivo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use