Kampuni ya Facebook ambayo inamiliki mitandao ya kijamii mbalimbali, hivi karibuni ilizindua sehemu mpya ya kuwaruhusu watumiaji wake kufuatilia taarifa kuhusu virusi vya corona kwenye mtandao wa Facebook.
Toka ilipo anzishwa takribani mwezi mmoja uliopita sehemu hiyo ilikuwa inapatikana kwenye nchi nyingi za jirani na ilikuwa bado haijawezeshwa kwa hapa nchini Tanzania. Lakini kuanzia siku ya leo sehemu hiyo inasemekana kuanza kuonekana rasmi kwa watumiaji wa Tanzania.
Kupitia sehemu hiyo mpya utaweza kupata taarifa mbalimbali kutoka tovuti ya wizara ya Afya nchini Tanzania, ikiwa pamoja na kurasa nyingine zilizozo thibitishwa kama kurasa ya Elimu ya Afya, kurasa ya CDC Africa, UNICEF TANZANIA pamoja na kurasa nyingine za muhimu kama World Health Organization (WHO).
Sehemu hiyo pia inakuja na taarifa za jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (Common Prevention Tips) ikiwa pamoja na njia salama za kujikinga kwa kufuata kanunuzi za wataalamu wa afya ikiwa pamoja na taarifa nyingine za muhimu.
Kwa sasa unaweza kutembelea sehemu hiyo kupitia app ya Facebook au kwa kutumia kompyuta yako kwa kufuata link hapa chini. Pia unaweza kupata sehemu hii kupitia sehemu ya Explore ndani ya App ya Facebook pamoja na tovuti ya Facebook.