Kampuni ya Facebook hivi karibuni inatarajia kuzindua mfumo mpya ambao utaweza kuzuia watu au akaunti mbalimbali kutumia picha za watu wengine ambazo zina haki miliki (copyrighted).
Mfumo huo mpya ambao utaweza kutumiwa na mtu yoyote, utaweza kusaidia watu kuzuia picha zao kutumika kwa kutuma maombi ya kuondoa picha hizo moja kwa moja kupitia facebook ambapo picha hizo zitaondolewa kwenye mitandao yote ya Facebook ikiwa pamoja na Instagram.
Sehemu hiyo mpya kwa sasa tayari imesha anza kutumika na kampuni mbalimbali ambazo facebook haijazionisha kwenye taarifa yake.
Kutumia sehemu hiyo mtumiaji anatakiwa kutuma file lenye format ya CSV, lenye maelezo yote ya haki miliki ya picha hiyo ikiwa pamoja na maelezo ya wapi haki miliki hiyo inatakiwa kuwekwa, yaani ni kwenye nchi gani ambapo unataka picha hiyo iweze kuondolewa.
Kwa sasa sehemu hiyo bado iko kwenye majaribio kwa watu wa chache na pengine unaweza kuona sehemu hii kabla ya mwaka huu kuisha. Kwa sasa kama unataka kutuma maombi ya picha yako kuondolewa kupitia mtandao wa Facebook na Instagram, unaweza kutumia fomu ya IP Reporting hapa. Kujua zaidi kuhusu sehemu hii endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.