Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Application Maarufu ya ES File Explorer Yaondolewa Play Store

App hii ni maarufu sana na inasemekana kuwa na Download zaidi ya Milioni 1
Application Maarufu ya ES File Explorer Yaondolewa Play Store Application Maarufu ya ES File Explorer Yaondolewa Play Store

Hivi karibuni kume kuwa na wimbi la apps mbalimbali kuonekana zikipotea kutoka kwenye soko la Play Store kwa sababu mbalimbali ikiwa pamoja na kukiuka vigezo na masharti ya utumiaji wa huduma za Google pamoja na kusemekana kutokuwa salama.

Hata hivyo Google imetuma barua pepe kwa wabunifu wote wa apps kupitia Play Store ili kuwataka kujua kuhusu mabadiliko mapya yanayokuja yatakayofanya apps kuchunguzwa zaidi kabla ya kuruhusiwa kuwekwa Play Store.

Advertisement

Sasa kutokana na mabadiliko hayo, app maarufu ya ES File Explorer imeonekana kuondolewa kwenye soko la Play Store bila wabunifu wa app hiyo kutoa sababu ya app hiyo kuondolewa kwenye soko hilo. Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya xda developers inasemekana app ya ES File Explorer imeondolewa kwenye soko hilo kutokana na kukiuka baadhi ya vigezo na masharti ya kutumia huduma za matangazo za Admob, ikiwa pamoja na kusemekana kutokuwa salama kwa asilimia 100.

App ya ES File Explorer ilikuwa ni app bora ya file manager hadi hapo ilipouzwa kwa kampuni ya kichina ya DO Global ambayo inamiliki app nyingi maarufu kama vile Du battery na app nyingine nyingi. Hata hivyo apps zaidi ya 100 ambazo zimetengenezwa na kampuni hiyo ya kichina kwa sasa zimeondolewa kwenye soko la Play Store huku apps hizo ziki kadiriwa kuwa na idadi ya jumla ya download zaidi ya milioni 600 kwa pamoja kabla ya kuondolewa Play Store.

Application Maarufu ya ES File Explorer Yaondolewa Play Store

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali inasema kuwa uwezekano wa app ya ES File Explorer kurudi kwenye soko la Play Store ni mkubwa hivyo huwenda app hiyo ikarudi kwenye soko hilo siku za karibuni. Kwa sasa kama unatafuta app nzuri ya File manager unaweza kujaribu apps za FX File Explorer, MiXplorer, au Solid Explorer ambazo zote hizi zinapatikana kupitia Play Store

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu app hii ya ES File Explorer ambayo inaonekana kupendwa zaidi na watumiaji wa wengi wa simu zilizopo rooted, hakikisha una tembelea Tanzania Tech kila siku tutakupa taarifa pindi app hiyo itakapo rudi kwenye soko la Play Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use