Ni kweli kwamba kwa sasa simu zimekua za aina nyingi sana, pamoja na kuwa na simu hizo zenye sifa na uwezo mbalimbali, bado kunalo tatizo la simu hizo kudumu na chaji. Kuliona hilo sasa inakuja simu ya Energizer Power Max P20, simu hii inauwezo wa kudumu na chaji pengine kuliko simu yoyote ili ambayo tumewahi kuizungumzi mpaka sasa.
Simu hii ya Energizer Power Max P20, inakuja na Battery kubwa yenye uwezo wa 4,000mAh Battery ambayo inaiwezesha simu hii kudumu na chaji kuanzia siku 31 bila kuchaji. Kwa upande mwingine, simu hii inauwezo wa kudumu na chaji kuanzia masaa 40 endapo unatumia simu hiyo kuongea mfululizo bila kupumzika.
Mbali na uwezo wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu, Energizer Power Max P20 pia inakuja na sehemu maalumu ya kuwezesha kuchaji simu nyingine yaani kifupi ni kuwa, unaweza kutumia simu hii kama Power Bank ya kuchaji simu nyingine.
Mbali na hayo simu hii inakuja na kioo cha inch 2.8-inch chenye resolution ya 240x320px display na inatumia line mbili za dual-SIM. Energizer Power Max P20 pia inakuja na sehemu ya kuweka memory card ambayo inauwezo wa kutumia memory card hadi ya GB 32, pamoja na kamera ya VGA yenye Megapixel 3. Vilevile simu hii inayo FM Radio pamoja na MP3 Music Player, bila kusahau simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa MB 32 pamoja na processor ya Spreadtrum SC6531E inayo saidiwa na RAM ya MB 4.
Bado kampuni nyingi za simu zina pambana kuja na simu zenye uwezo wa kudumu na chaji zaidi. kwani hata hivi karibuni tuliona simu janja ya Blackview P1000 ambayo yenyewe ilikuwa inauwezo wa kudumu na chaji kwa siku 7 kutokana na ukubwa wa battery yake yenye uwezo wa 11,000mAh.