Habari njema kwa wapenzi na watumiaji wa Emoji, wataalamu kutoka Unicode Consortium ambao ndio wabunifu na watengenezaji wa Emoji wametangaza ujio wa Emoji mpya zaidi ya 150 mwaka huu 2018.
Emoji hizo ambazo tayari zimesha ruhusiwa kuanza kutumika kama toleo jipya la Emoji Unicode 11.0 zinategemewa kuanza kutumika kwenye simu janja zenye uwezo wa emoji kuanzia mwezi wa nane au wa tisa mwaka huu.
Zifuatazo ni baadhi ya Emoji hizo mpya ambazo zitakuja kwenye mifumo yote ya simu janja yaani iOS na Android baadae mwaka huu.
Emoji hizi mpya hazitakuja kama sehemu ya toleo jipya la mifumo ya Android au iOS bali zitakuja kwa watumiaji wote wenye simu zenye uwezo wa kuonyesha, kutuma na kupokea Emoji hasa toleo hilo jipya la Unicode 11.0.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.