Elon Musk ni mkurungenzi mtendaji na mgunduzi wa kampuni za Tesla pamoja na Space X, Hizi ni moja kati ya kampuni kubwa sana duniani ambapo Tesla ni kampuni inayo tengeneza magari ya kifahari yanayotumia umeme na SpaceX ni kampuni inayo jihusisha na utengenezaji ndege pamoja na kutoa huduma za usafiri wa anga. Kampuni zote hizi zinamilikiwa na Elon Musk.
Sasa katika hali ya kushangaza kidogo, hapo jana mkurugenzi wa makampuni hayo alifuta kurasa za facebook za kampuni zake hizo kutokana na mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter kumshinikiza Afanye hivyo. Musk alijibu baadhi ya Twitter ambazo zimeandikwa “Delete SpaceX page on Facebook if you’re the man?” ikiwa na maana “futa kurasa ya facebook ya SpaceX kama wewe ni mwanaume?”
Musk kupitia ukurasa wake huo alijibu kwenye tweet hiyo “I didn’t realize there was one. Will do.” ikiwa na maana “Sikujua kwamba kuna moja. Nita fanya.” yaani akiwa na maana akujua kama kuna kurasa ya facebook ya kampuni yake ya SpaceX huku pia akikubali kuifuta. Hata hivyo haikupita muda mtu mwingine alimshinikiza kufuta kurasa ya Tesla kwa kusema, “this should be deleted too right?” akiwa na maana “na hii pia ingefutwa” huku akiwa ameweka picha ya ukurasa wa facebook wa kampuni ya Tesla, Musk hakuchukua muda alijibu kwa kuandika, “Definitely. Looks lame anyway.” akiwa na maana “Hakika. Inaonekana vibaya hata hivyo.”
Baada ya muda kidogo kurasa zote za kampuni hizo zilipotea kwenye mtandao wa Facebook na kuacha watu wakishangaa. Kurasa hizo za makampuni hayo ya Tesla na SpaceX zote zilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni moja (1M) kwa kila moja na zilikuwa tayari ziko Verified.
Hatua hii inakuja kwa sababu ya kuanzishwa kwa hashtag ya #deletefacebook kwenye mtandao wa Twitter, ambayo ilianzishwa baada ya kuanza kwa sakata la kampuni ya Cambridge Analytica kusemekana kuwa ilitumia data za watumiaji wa mtandao wa facebook zaidi ya milioni 50 kinyume na sheria ili kumsaidia raisi Donald Trump kushinda uchaguzi wa uraisi ulio fanyika mwaka 2016.