Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ecobank Yaja na Suluhisho la Manunuzi ya Mtandaoni Bila Kadi

Hivi karibuni utaweza kufanya manunuzi ya mtandaoni bila kutumia kadi
Ecobank Ecobank

Manunuzi ya mtandao yamekua ya shida sana hapa Tanzania tena hii huwa ngumu zaidi kama huna kadi maalum ya benk iliyowezeshwa na huduma ya manunuzi ya mtandaoni, lakini kwa mara ya kwanza hapa Tanzania bank ya Ecobank imekuja na suluhisho.

Bank hiyo ambayo ipo hapa Tanzania na nchi nyingine 36 Afrika imekuja na huduma hiyo mpya kabisa ya kuwezesha malipo ya mtandaoni bila kutumia kadi yaani Visa na MasterCard. Badala yake sasa utaweza kununua kitu kupitia mitandao ya nje ya Tanzania kwa kutumia programu ya simu au mobile app.

Advertisement

Mkurugenzi mpya wa Ecobank, Mwanahiba Mzee amesema kuwa, huduma hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo na itakuwa sehemu ya uboreshaji wa programu ya sasa ya Ecobank mobile app ambayo inarahisisha ufanyaji miamala kutoka na kwenda benki na akaunti za fedha za simu.

Mzee ambaye benki yake ipo katika kundi la pili la benki (Tier 2), amesema wataendelea kuwezesha ukuaji wa uchumi kwa kutoa mikopo itakayosaidia wafanyabiashara kufikia malengo yao na hasa biashara zinazovuka mipaka na uuzaji wa mazao.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Mwananchi

5 comments
  1. Dah itakuwa poa sana sasa wananza lini na maelezo ya jinsi ya kuitumia natumaini yatawekwa hapa kazi nzuri sana Tanzania Tech.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use