Kipindi cha siku kuu za kufunga mwaka kimekaribia, watu wengi mbalimbali kipindi hichi wanapenda kutembelea kwenye maduka mbalimbali ili kununua zawadi mbalimbali kwaajili ya ndugu na jamaa.
Katika hali ya kushangaza kidogo huko marekani kumezuka wimbi la vijana wanovamia maduka mbalimbali ya kampuni ya Apple na kuchukua bidhaa mbalimbali zilizoko kwenye maduka hayo. Tarehe 25 ya mwezi November wezi watatu walivamia duka moja la Apple huko marekani wakiwa hawana sila yoyote na kuchukua simu zilizokua juu ya meza kama maonyesho kwa wateja, katika hali ya kushangaza fanyakazi wa duka hilo walikua wamesimama tu bial kuchua hatua yoyote.
Tarehe 29 November wezi hao walirudi tena kwenye duka hilohilo na kuchukua tena bidhaa zilizokua juu ya meza na kuondoka haraka ndani ya sekunde 15 pekee. Kama kawaida Wafanyakazi wa duka hilo kwa mara nyingine walikua wakishangaa, hadi mtu mmoja alipoamua kuzuia mlango huku akionekana kupiga simu polisi.
Hata hivyo Polisi wa mjini San Francisco wanaendelea kuwatufuta watu hao na kuomba msaada kwa wananchi wake kwa kutoa video hiyo ya waalifu hao iliyochukuliwa na security camera iliyokua ndani ya duka hilo.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.