Hivi karibuni mtandao wa instagram umezindua sehemu mpya ya reels ambayo inakuruhusu kupakia video na kuweka sauti au muziki kama ilivyo app ya TikTok. Sehemu hiyo kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wote wa mtandao wa instagram kote duniani.
Kama bado huja anza kutumia sehemu ya reels unaweza kupata sehemu hii moja kwa moja kupitia sehemu ya kamera inayopatikana juu upande wa kushoto pale unapkuwa kwenye ukurasa wa explore, bofya hapo kisha utaona sehemu imeandikwa reels, bofya hapa kuanza kurekodi au kuweka video.
Sasa, baada ya kuanza kutuma sehemu hii ni wazi kuwa lazima utaweza kuona video nzuri za kufurahisha ambazo pengine ungehitaji kuwa nazo kwenye simu yako. Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ya kudownload video za reels ikiwa pamoja na video za IGTV.
Jinsi ya Kudownload Video za Reels
Kwa kuanza hakikisha unatumia simu ya Android, kisha moja kwa moja unaweza kupakua app ya FastSave for Instagram ambayo inapatikana kupitia soko la Play Store. Unaweza kupakua app hiyo kwa kubofya hapo chini na utapelekwa moja kwa moja kwenye soko la Play Store.
Kama kuna tatizo lolote kwenye link hiyo basi unaweza kutumia link hii hapa kuweza kupakua app hii moja kwa moja kwenye soko la Play Store.
Baada ya kuinstall, moja kwa moja fungua app hiyo kisha nenda kwenye app ya instagram na kisha kwenye sehemu ya explore au kwenye profile ya mtu na utaweza kuona sehemu ya reels. Bofya video unayotaka kudownload kisha bofya kutufe cha share.
Kisha chagua share to na moja kwa moja chagua app ya FastSave ambayo itakuwa kwenye list ya app ambazo unaweza kushare.
Baada ya hapo subiria wakati app hiyo ikidownload reels kwenda kwenye simu yako, hakikisha unabaki kwenye ukurasa huo mpaka hatua zote kukamilika.
Baada ya hapo utaweza kuona video zote ulizopakua kupitia ndani ya app hiyo, au unaweza kuangalia kwenye Gallery ya simu yako.
Jinsi ya Kudownload Video za IGTV
Kama unataka kudownload video za IGTV, pia unaweza kufuata hatua kama hizi hapo juu lakini hakikisha unaingia kwenye akaunti ya mtu kwenye sehemu ya IGTV au kwenye video yoyote ya IGTV.
Baada ya hapo bofya share to na kisha chagua app ya Fast Save na moja kwa moja subiri mpaka app imalize kusave video hiyo na moja kwa moja utaweza kupata video ya IGTV uliyokuwa unataka kwenye simu yako.
Na hiyo ndio njia fupi na rahisi ambayo unaweza kutumia kudownload video za IGTV, kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unasoma hapa jinsi ya kudownload video za TikTok bila kuwepo kwa alama ya username kwenye video.
Haya ni majaribio