Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine (Updated)

Jifunze hapa njia nyingine ya kuforwad meseji kutoka simu moja kwenda nyingine
Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine (Updated) Jinsi ya Kudivert SMS Kwenda Simu Nyingine (Updated)

Kama wewe ni msomaji wa Tanzania Tech basi lazima unajua kuwa tulishawahi kuzungumzia njia ya kuforward SMS kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kama bado hufahamu kuhusu njia hiyo unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua.

Lakini baada ya kuonyesha njia hiyo watu wengi walisema kuwa njia hiyo inakuja na mambo mengi na pengine inaweza kumshinda mtu asiye na ujuzi wa kutumia simu ya Android.

Advertisement

Kuliona hilo hivi leo nimekuletea njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi ambayo itakusaidia ku forward meseji kutoka namba moja ya simu kwenda namba nyingine. Kumbuka njia hii inaweza kufanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android 5.0 na kuendelea. Kama unatumia Android 4.0 basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutaleta njia hii kupitia mfumo huo siku za karibuni.

Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizi rahisi na fupi. Kwa kuanza hakikisha una download app ya SMS Forward kupitia link hapo chini. App hii haipatikani kupitia soko la Play Store hivyo hakikisha unapakua kupitia link hapo chini.

Download App ya SMS Forward

Baada ya kudownload na ku-install vizuri app hii sasa unaweza kuendelea kwa kufanya setup hizi rahisi. Baada ya kufungua app hii bofya sehemu ya jumlisha iliyopo chini katikati.

Baada ya hapo utaletewa ukurasa ambapo unatakiwa kuchagua namba ambayo meseji zikitumwa kwenye simu ambayo ume install app, namba hiyo ndio itapokea meseji hizo.

Baada ya hapo bofya sehemu ya SMS forward kwani app hii inaweza kuforward hadi notification. Baada ya hapo unatakiwa kuruhusu permission kwenye app hiyo kisha moja kwa moja malizia setup.

Baada ya hapo basi moja kwa moja kila meseji ambayo simu yako itakuwa inapokea basi moja kwa moja utakuwa unaweza kupata kupitia namba ambayo uliweka awali.

Kitu cha muhimu ni kuhakikisha simu inayo pokea meseji inayo SMS au muda wa maongezi kwa ajili ya kutuma SMS hiyo kwenye namba ya pili.

Kama unataka njia yenye uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi basi unaweza kuangalia njia ya kwanza ambayo inakupa uwezo wa kupokea meseji kutoka kwenye kundi la watu au hata mtu mmoja mmoja, pia unaweza ku-forward meseji za watu ambao hata awapo kwenye phonebook yako ikiwa na mambo mengine.

Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha una soma hapa jinsi ya kupokea SMS kupitia app ya Telegram.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use