Hizi Ndio Kompyuta Bora za Desktop za Kununua Mwaka 2019

Kama Unatafuta Kompyuta za Desktop kwaajili ya matumizi ya ofisi yako au Kazi nyingine Soma makala hii
Kompyuta za desktop bora Kompyuta za desktop bora

Ikija katika swala zima la kununua kompyuta aina ya desktop viko vitu vya msingi vya kuangalia baadhi ya vitu hivyo vya msingi ni nguvu ya kompyuta, aina ya kompyuta, size ya kompyuta pamoja na jina la kompyuta au brand. Yote haya ni yamuhimu sana yote haya tuta yazungumzia yote kwenye makala zingine zinazokuja kwa leo twende tukazichambue kompyuta bora za desktop za kununua mwaka huu 2019.

1. HP Envy Curved 34-A051

Advertisement

HP Envy Curved 34-A051

HP Envy Curved 34-A051 ni moja kati ya kompyuta ya kisasa kabisa yenye sifa bora na yenye muonekano mzuri kama unatafuta kompyuta ya desktop bora yenye muonekano na yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi HP Envy Curved 34-A051 ni kompyuta yako.

Sifa

  • CPU: Intel Core i7-6700T
  • Graphics: Nvidia GeForce GTX 960A
  • RAM: 12 GB
  • Storage: 1TB HDD, SSD
  • Communication: Wireless: 902.11ac, Bluetooth 5.0
  • Dimensions Screen 34 inches, Resolution 3440 x 1440

2. Apple iMac Yenye 5K Retina display

Apple iMac

Kompyuta hii ni moja kati ya kompyuta bora kabisa za kununua pale unapowaza kununua dektop kwani kompyuta hii haitaji wanya nyingi kwani kila kitu kipo kwenye kioo cha kompyuta hii unachoitaji ni adapter yake na hapo utakua tayari uko tayari kutumia kompyuta yako.

Sifa

  • CPU: Intel Core i5-4260U
  • Graphics: Intel Iris Graphics 5100
  • RAM: 4GB 16GB
  • Storage: 500GB HDD
  • Communication: Wireless: 802.11ac, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 196 x 196 x 36mm

3. Apple iMac Yenye 4K Retina display (21.5-inch, Mwaka 2015)

iMac Desktop

Ikiwa na kioo angavu pamoja na uwezo wa hali ya juu kompyuta hii kutoka kampuni ya apple ni moja kati ya kompyuta za aina yake za mwaka 2015, 2016. Kompyuta hii inauwezo wa hali ya juu sana na nimoja kati ya zile kompyuta wanazo ziita One in One Kompyuta.

Sifa

  • CPU: Intel Quad-Core i5 (Turbo Boost up to 3.6GHz)
  • Graphics: Intel Iris Pro Graphics 6200
  • RAM: 8GB 1867MHz LPDDR3
  • Storage: 1TB Serial ATA Drive @ 5400RPM
  • Communication: Wireless: 802.11ac, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 45cm x 52.8cm x 17.5cm

4. Dell Inspiron 3000

Dell Inspiron-650-80

Pale inapokuja katika tower desktop kompyuta dell ni moja kati ya makampuni yanayo heshimika sana kwa kutengeneza desktop bora Dell Inspiron 3000 ni moja kati ya kompyuta bora za dektop kompyuta hii ina kila kinachoijaika kuanzia nguvu ya kufanya kazi mpaka muundo hii ni moja kati ya desktop kompyuta ambazo ni vyema kuanazo kwa matumizi ya ofisini.

Sifa

  • CPU: Intel Core i3-4170
  • Graphics: Intel HD Graphics 5000
  • RAM: 8GB
  • Storage: 1TB hard disk
  • Communication: Dell Wireless-N 1705, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 178 x 388 x 431mm

5. Apple Mac mini

Apple Mac mini

Apple Mac mini ni moja kati ya kompyuta za kisasa kabisa zenye kukupa uwezo wa kutumia nguvu halisi ya kompyuta ya desktop kutoka kwenye kifaa kidogo saizi ya viganja vya mikono yako, kompyuta hii ina uwezo mkubwa kuliko hata kompyuta nyingi ambazo ni kubwa.

Sifa

  • CPU: Intel Core i5-4260U
  • Graphics: Intel Iris Graphics 5100
  • RAM: 4GB
  • Storage: 500GB hard disk
  • Communication: Wireless: 802.11ac, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 196 x 196 x 36mm

6. Asus K31ADE

Asus K31 1-650-80

Pale unapofikiria kununua desktop ni vyema ukatafuta kompyuta ambayo inakidhi mahitaji ya kazi ile amabayo unaenda kufanya hivyo basi kama unatafuta kompyuta yenye nguvu pamoja na uwezo mkubwa wa kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu Asus K31ADE ni kompyuta bora kwako kwani ina sifa ambazo ni bora kabisa.

Sifa

  • CPU: Intel Core i3-4170
  • Graphics: Intel HD Graphics 5000
  • RAM: 4GB
  • Storage: 1TB hard disk
  • Communication: 802.11ac
  • Dimensions (W x D x H): 180 x 350 x 390mm

7. Acer Revo One RL85

Acer Revo One RL85 hero-650-80

Acer Revo One RL85 ni moja kati ya kompyuta za kisasa kabisa kutoka kampuni ya Acer kwa tanzania ni baadhi ya maduka machache sana yenye kompyuta hii ila kwa uhakika zaidi ili kupata kompyuta hii ni vyema kuiagiza mtandaoni moja kwa moja.

Sifa

  • CPU: Intel Celeron 2957
  • Graphics: Intel HD Graphics
  • RAM: 4GB
  • Storage: 2TB hard disk
  • Communication: 802.11n, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 107 x 107 x 220mm

8. Acer Chromebase DC221HQ

Acer Chromebase DC221HQ

Kwa sasa komyuta nyingi zinakuja zinakuja kwa jina la Chromebook kompyuta hizi zinakuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha programu za kutoka kwenye mfumo wa android, pia kompyuta hizi zinakuwa na uwezo mkubwa sana hasa katika kazi za utengenezaji wa programu au app developmet kama wewe ni developer na unatafuta kompyuta yenye uwezo mzuri wa kufanya hivyo kompyuta hii ni kwaajili yako.

Sifa

  • CPU: 2.1 GHz Nvidia Tegra K1
  • RAM: 4GB 1600MHz DDR3 SDRAM
  • Storage: 1TB 5,400rpm HDD
  • Communication: 802.11n Wi-Fi, Gigabit Ethernet, Bluetooth 4.0
  • Dimensions Screen Size 21.5 inches, LCD Widescreen, Resolution 1920 x 1080

9. HP Pavilion Mini

HP Pavilion Mini-650-80

Hii ni moja kati ya zile mini desktop kompyuta ambazo haziitaji kuchukua nafasi kubwa katika meza ya ofisi yako au hata meza ya chumbani kwako, ikija katika HP Pavilion Mini komyuta hii ni maalumu kwa matumizi madogo madogo ya kawaida kwani sifa zake ni za kawaida na uwezo wake pia ni mkubwa kwenye kufanya kazi za kawaida kama kuandaa dokumenti na mambo kama hayo.

Sifa

  • CPU: 1.9GHz Intel Core i3-40255U
  • RAM: 4GB 1600MHz DDR3 SDRAM
  • Storage: 1TB 5,400rpm HDD
  • Communication: 802.11n Wi-Fi, Gigabit Ethernet, Bluetooth 4.0
  • Dimensions (W x D x H): 144mm x 144mm x 52mm

Na hizi ndio baadhi ya kompyuta bora kabisa za desktop za kununua mwaka huu 2016, kama unataka kujua bei za kompyuta hizi  tuandikie kwenye maoni yako hapo chini na sisi tuta update list hii kwa kuweka bei za kila kompyuta kwa pesa ya kitanzania, pia kama ungepend kujua ni wapi pa kununua kwa hapa tanzania vyote tuandikie maoni nasi tutaongeza vitu hivyo.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

11 comments
  1. Habar asanten kwa maelezo hayo ila nilitaka kujua bei ya computer ambazo mmeziorozesha hapo.

  2. Naomba kutumiwa being za kompyuta ambazo umerodhozesha katika email yangu na mnipe maelekezo mpo pande zipi kwa kufika

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use