Kampuni ya Dell imeuanza mwaka 2018 kwa kutoa toleo jipya la laptop yake ya Dell XPS 13 (2018), laptop hiyo ambayo ni muendelezo wa matoleo ya laptop za XPS sasa inakuja na maboresho zaidi na muonekano mpya.
Laptop hiI ya Dell XPS 13 (2018) ambayo imetoka mapema kabla ya mkutano wa vifaa vya kieletroniki CES 2018, inakuja na maboresho ya muonekano wake pamoja na kuongezewa baadhi ya vitu kama vile uwezo wa kioo cha 4K pamoja na rangi nyeupe na uwezo wa kuzuia uchafu.
Kama ulikuwa huijui laptop za XPS 13, hizi ni laptop ambazo ni bora zaidi kutoka kampuni ya Dell na zimekuwa kwenye list ya laptop bora kwa miaka mingi kwenye nchi mbalimbali. Mbali na laptop hii kusifika kwa ubora kwa miaka mingi, mwaka huu 2018 Dell imeongeza mvuto wa laptop hiyo na kufanya laptop hiyo kuwa nzuri zaidi na bora kwa muonekano na uwezo.
Dell XPS 13 ya Mwaka 2018 inakuja ikiwa imeongezewa wembamba ambao unafanya laptop hiyo kuwa na uzito wa pound 2.67 sawa na Kilogram 1.21, Vilevile laptop hii sasa inakuja na kioo cha kisasa cha Dell’s “InfinityEdge” ambacho kinakuwa na kingo nyembamba zaidi ikiwa imepungua asilimia 23 ukilinganisha na matoleo ya laptop za XPS ya miaka iliyopita.
Mbali na hayo kioo hicho pia kimeongezewa teknolojia mpya na sasa kitakuwa na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye teknolojia ya 4K huku ikiwa inawezeshwa na kusaidiwa na teknolojia mpya ya Dell Cinema. Dell pia imeweka aina mpya za vipoozeo vya joto kwenye laptop hiyo na kufanya uweze kutumia laptop hiyo kwa muda mrefu bila kupata joto sana.
Dell pia imeboresha laptop ya XPS 13 (2018) kwa upande wa sauti kwa kuongezea teknolojia hiyo ya Dell Ciname ambayo inaleta uwezo wa Waves Maxx audio enhancements ambayo inaweza kutoa sauti nzuri na bora zaidi. Pia laptop hiyo imeongezewa processor yenye nguvu zaidi ya 8th-Generation Processor.
Kifupi mabadiliko ya uwezo yalioko kwenye laptop mpya ya Dell XPS 13 (2018) ni yafuatayo –
- Processor – 8th-generation Intel quad-core i5-8250U au i7-8550U processor
- RAM – 4GB au 8GB RAM (1,866MHz) au 16GB RAM (2,133MHz)
- Ukubwa wa Hard Disk / SSD – 128GB SATA SSD au 256GB, 512GB au 1TB PCIe SSD
- Uwezo wa Graphics – Intel UHD Graphics 620
Laptop hiyo mpya ya Dell XPS 13 (2018) inakuja ikiwa na bei mpya ya dollar za marekani hadi $1000 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 2,250,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo (kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania).
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
Bonge la kompyuta dooh