Mwaka 2020 tayari umeanza na kama unakumbuka kila mwanzo wa mwaka huwa dunia inakusanyika pamoja kuonyesha teknolojia mpya kwenye mkutano wa CES au (Consumer Electronics Show). Kwa mwaka huu mkutano huo unategemea kuanza rasmi hivi karibuni na tayari kampuni nyingine zimeanza kuzindua bidhaa zake mapema.
Kupitia mkutano huo wa CES 2020, Kampuni ya Dell imetangaza ujio wa laptop zake mpya za Dell XPS 13 pamoja na laptop mpya ya Dell Latitude 9510. Laptop hizi zote zinakuja na muonekano wa kisasa pamoja na sifa za kuwa laptop nyembamba zaidi lakini pia zenye vioo vikubwa na bora.
TABLE OF CONTENTS
Dell XPS 13
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, laptop mpya ya Dell XPS 13 (2020) imeboreshwa zaidi. Laptop hii mpya ya Dell XPS 13 inakuja ikiwa nyembamba zaidi, huku kioo chake kikiwa kimesogea zaidi na kupunguza kingo za pembeni na kufanya laptop hiyo kuonekana kama ni kioo kitupu au InfinityEdge.
Kwa nje Dell XPS 13 (2020) imetengenezwa kwa aluminiam, nyuzi za kaboni, pamoja na kioo cha Gorilla Glass ambacho akipasuki kirahisi. Laptop hizi zinakuja kwa matoleo matatu yenye vioo tofauti kama inavyo weza kuonekana hapo chini.
Kioo | Inch 13.4 yenye 4K touch display Inch 13.4 yenye FullHD touch display Inch 13.4 yenye FullHD display |
Viunganishi | 2x Thunderboltâ„¢ 3 1x microSD card reader v4.0 1x 3.5mm headphone/microphone combo jack; 1x TypeC to USB-A v3.0 adapter |
Battery | 52Whr |
Graphics | Intel UHD Graphics; Intel Iris Plus Graphics |
Bei | starts at $999.99 = TZS 2,300,000 bila kodi |
Processor | Up to 10th-gen Intel Core i7 1065G7 up to 3.9GHz |
RAM | Up to 32GB LPDDR4x |
Dell Latitude 9510 (2020)
Kwa upande wa Dell Latitude 9510, laptop hii inasemekana kuja na sifa moja kubwa ambayo kwa mujibu wa Dell ni sifa ambayo laptop nyingine zote za inch 15 hazina sifa hizo. laptop hiyo inasemekana kudumu na chaji kuliko laptop nyingine za Inch 15.
Laptop hii hpia inakuja na uwezo wa 5G kwani inakuja na anntena yenye uwezo huo ikiwa imefungwa ndani ya laptop hiyo. Mbali na hayo Dell Latitude 9510 inakuja na WiFi 6 ambao ni mfumo mpya wa teknolojia ya WiFi. Sifa nyingine za Dell Latitude 9510 ni kama zifuatazo.
Kioo | 15-inch FHD touch display; 15-inch FHD display |
Processor | Up to 10th-gen Intel Core i7 |
RAM | Up to 16GB LPDDR3 |
Graphics | Intel UHD Graphics |
Uhifadhi | Up to 1TB NVMe SSD |
Battery | Up to 88Whr |
Viunganishi | 1 x USB 3.1 Gen 1; 2 x Thunderbolt 3; 1 x HDMI 2.0; 1x external uSIM card tray; 1 x uSD 4.0 Memory card reader; 1 x Optional Contacted SmartCard Reader; 1 x Optional Touch Fingerprint Reader in Power Button |
Bei | $1,799 = TZS 4,134,000 bila kodi |
Kwa mujibu wa Dell, Laptop hizi zinatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, huku Dell XPS 13 (2020) ikitarajiwa kuingia sokoni mwezi huu januari na Dell Latitude 9510 yenyewe ikitarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu 2020.