Kwa wapenzi wa mtandao wa YouTube hivi karibuni utaweza kutumia app ya YouTube ya Android ikiwa kwenye rangi ambayo ni nzuri kwa macho yako hasa wakati wa usiku.
Dark Theme ni sehemu ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kupatikana kupitia tovuti ya mtandao wa Youtube na baadae kuja kwenye app ya YouTube ya iOS na sasa hivi karibuni imekuja rasmi kwenye app ya Android. Kama ulikuwa hujui faida za sehemu hiyo labda nikujuze kidogo.
Kwa kawaida vifaa vya kielektroniki hasa kompyuta, simu, tablet na vingine kama hivyo vinakuja na screen au vioo ambavyo huonyesha rangi mbalimbali. Lakini kwenye rangi hizo kuna rangi ambazo sio nzuri kwenye macho ya binadamu na ndio maana tulisha ongelea sheria ya 20,20,20 ambayo inasaidia kulinda macho yako dhidi ya rangi hizo au miale hatari ya mwanga inayotolewa na vifaa hivyo vya kielektroniki.
Sasa kwa upande mwingine Dark Mode inasaidia sana kuondoa hiyo miale ambayo kwa namna moja ama nyingine inapatikana kwa wingi kwenye rangi nyeupe ambayo ndio hutumika kwa asilimia kubwa kwenye programu zinazokuwa ndani ya vifaa hivyo, kwa hiyo basi kama programu fulani unayopenda kuitumia sana inayo sehemu ya Dark Mode basi ni vyema kuitumia mara kwa mara hasa wakati wa usiku. Sasa ili kutumia sehemu hii kwenye app ya YouTube unaweza kufuata hatua hizi.
Fungua App ya Youtube ya Android kisha bofya kwenye picha ya akaunti yako inayopatikana juu kulia, baada ya hapo bofya Settings kisha bofya General kisha bofya sehemu imeandikwa Dark Theme. Baada ya kubofya hapo moja kwa moja utaona application ya YouTube imebadilika rangi na kuwa rangi nyeusi.
Sehemu hii tayari inapatikana kwenye app ya YouTube hivyo kama bado uja-update app ya YouTube fanya hivyo sasa kupitia soko la Play Store. Vilevile pia sehemu hii inapatikana pia kwenye app ya Tanzania Tech unaweza kuiwasha kupitia sehemu hiyo kupitia sehemu ya profile kisha bofya Soma Usiku.