Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Zifuatazo ni baadhi ya dalili zinazo onyesha kuwa inawezekana simu yako imeadhiriwa na Virus
virus virus

Ni wazi kuwa kadri teknolojia inavyozidi kukuwa pia yapo mambo ambayo yanakuwa pamoja na teknolojia ambayo pengine sio mazuri, hasa kwenye ulimwengu huu wa Data.

Pengine unaweza kujiuliza kwa nini simu yako iadhiriwe na malware au virus.? Jibu ni moja tu “Data”, katika ulimwengu huu ambapo biashara nyingi zinafanyika mtandaoni ni wazi kuwa data ni kitu cha muhimu sana, umuhimu huu unapelekea baadhi ya watu au makampuni kukusanya data kwa njia isiyokuwa sahihi, moja ya njia hizo ni kuweka malware au virus kwenye simu yako.

Advertisement

Malware hizo au virus hutoa data kutoka kwenye simu yako na kuzituma kwenye server mbalimbali kwaajili ya matumizi ya kibiashara au kwaajili ya ku-uza data hizo kwa makampuni makubwa, data hizo huweza kuwa apps unazo tumia mara kwa mara, sehemu unazofikia, mtandao unaotumia, na mambo mengine mengi ambayo ni ya binafsi.

Kuliona hili leo nimekutea makala ambayo itaenda kukusaidia kuweza kujua kwa awali kama simu yako imeadhiriwa na virus au Malware. Kumbuka dalili hizi ni baadhi tu inawezekana kuwepo kwa dalili zingine ambazo hazipo hapa. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.

Chaji Kupungua kwa Haraka Sana

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Kuna sababu nyingi za simu kupungua chaji kwa haraka, lakini kama simu yako ni mpya, au haina mda mrefu na pia sio mbovu lakini chaji inapungua kwa haraka kupita kiasi basi inawezekana simu yako imeadhiriwa na malware au virus. Mara nyingi hii husababishwa na malware hizo kufungua programu nyingi bila wewe kujua na kuchukua na ku-upload data mbalimbali.

Simu yako Kustaki Mara kwa Mara

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Pamoja na sababu hapo juu, programu nyingi zinapo funguliwa na malware husababisha simu yako kustack kila mara na hii huwa ni kwa sababu ya kutumika kwa kasi kwa RAM kwenye simu yako na kufanya ishindwe kufanya kazi vizuri inavyo takiwa.

Kukatika kwa Simu Mara kwa Mara

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Kukatika kwa simu hasa pale unapopiga wewe ni jambo la kawaida sana hasa hapa Tanzania, lakini kama simu yako inakatika sana hasa unapo piga simu wewe. Hii usababishwa na aina fulani ya Malware ambayo husikiliza simu zako.

Utaona Programu Ambazo Huku Wahi Kudownload

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Mara nyingi simu nyingi huwa na programu ambazo zinakuja na simu na pia kuna programu ambazo ume download, lakini ikitokea umekuta programu kwenye simu yako ambayo hujawahi kudownload na hata uki-uninstall hazitoki basi kuna uwezekano mkubwa simu yako tayari imesha athiriwa na virus au malware.

Simu Kuchukua Muda Kuwaka

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Simu kuchukua muda kuwaka ni jambo ambalo kwa sasa kwenye simu za siku hizi ni ngumu sana kutokea, hivyo kama unaona simu yako inachukua muda mrefu sana kuwaka basi anza kuchukua hatua za haraka kwani kuna uwezekano malware au virus zimeingia kwenye simu yako na hutumia muda kujiwasha kabla simu ya programu nyingine kwenye simu yako.

Kujiwasha kwa Bluetooth pamoja na WiFi

Dalili Simu Yako Imeadhiriwa na Malware au Virus

Kuna wakati Wifi na Bluetooth hujiwasha kwa bahati mbaya, lakini Kama kuna muda unakuta simu yako imejiwasha bluetooth pamoja na wifi au kimoja kati ya hivyo na hujashika simu yako kwa muda mrefu basi inawezekana kabisa simu yako hiyo ipo hatarini au tayari imeadhiriwa na virusi hivyo ni vizuri kufuata hatua zinazofuata hapo chini.

Jinsi ya Kuzuia Simu Kuwa Hacked

Ni wazi kuwa usalama wa mawasiliano binafsi ni kitu cha muhimu na kwa kuzingatia hilo basi ni vyema kuwa makini na kifaa chako cha mawasiliano.

Backup na Reset Simu Yako

Kama kwa namna yoyote unahisi simu yako imeadhiriwa na Virus au malware hatua ya kwanza ya muhimu ni kufanya backup na kureset simu yako moja kwa moja. Hakikisha hutumii backup hiyo kwenye simu yako hadi hapo utakapo thibitisha kuwa ni salama.

Tumia Programu za Kudhibiti Data

Pia unaweza kuhakikisha unatumia programu za kuzuia data kutumika na programu ambazo hutaki zitumie data, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kudownload na kutumia programu hizo ambazo zinaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kwani virus au malware nyingi hutumia internet kutoa data kwenye simu yako kwa kuthibiti data utakuwa umezuia malware hizo.

Tumia programu za Ulinzi

Zipo programu nyingi za ulinzi ambazo husaidia kuzuia au kuondoa aina mbalimbali za malware, lakini hizi ni nzuri kutumia kabla ya simu yako haija adhiriwa. Wakati mwingine unaweza kujaribu kutumia programu hizi hata simu yako inapokuwa imeadhiriwa, simu za siku hizi nyingi zinakuja na programu za ulinzi moja kwa moja, unaweza kutafuta kupitia sehemu ya Settings > Security.

Badilisha Password Kwenye Akaunti ya Goolgle

Kwa kawaida ni muhimu kubadilisha password angalau mara moja kwa mwaka, hii itakusaidia kuweza kulinda akaunti yako kama imeadhiriwa kwa namna yoyote, pia hakikisha password unayo tumia ni salama kwa asilimia 100.

Hizo tu ni baadhi ya dalili ambazo zinaweza kuonyesha kama simu yako imeadhiriwa na virus au malware mbalimbali, kumbuka hizi ni baadhi tu ya dalili, hivyo ni vizuri kuangalia tabia ya simu yako kama imebadilika ili kujua tatizo la simu yako. Kwa maujana zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech.

7 comments
  1. Comment*Cm yangu ni tecno h 5,karibu 90% ya hizo dalili inazo,swali ni je kuiflash au kufanyaje???Maana nishafanya back up zaidi ya mara moja ila tatizo halijaisha,bado ni vilevile.Mnijuze kwa msaada zaidi

  2. Asante Francis kwa kutembelea Tanzania tech, kumbuka kuwa makini katika kufanya backup unakuta unachukua na programu inayosababisha matatizo hayo, hivyo cha kufanya format simu yako kisha anza mwanzo usiweke programu za zamani bali jitahidi kuzidownload kwa upya, pia hakikisha unaweka antivirus kabla ya kuistall programu yoyote.

  3. kwa mfano:mwingine hana kompyuta inamaana hakuna uwezekano wa cm hiyohiyo kuifadha mafaili,nyimbo na video pale unapo resat cm yako?

  4. Habari simu yangu in vodafone 301 imeathiriwa na virus wa kutoka kwenye memory card ni fanyaje ili kuwaondoa?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use