Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Chupa za Soda za Kielektroniki za Coca Cola

Je wajua hizi ndio chupa za kwanza za Kielektroniki za Coca Cola
Zifahamu Chupa za Soda za Kielektroniki za Coca Cola Zifahamu Chupa za Soda za Kielektroniki za Coca Cola

Kampuni ya Coca Cola ni moja kati ya kampuni ambazo zinafanya ubunifu mkubwa sana hasa kwenye ulimwengu wa matangazo ya bidhaa zake. Utakubaliana na mimi kuwa, karibia kila tangazo la Coca cola linalo onekana hata hapa Tanzania, lina ubora wa hali ya juu na pengine linaweza kuwa halichoshi kuangalia kutokana na ubunifu au hadithi inayokuwa nyuma yake.

Hakini mwishoni mwa mwaka jana 2019, kampuni ya Coca Cola ilipiga hatua moja mbele kwa kutumia teknolojia zaidi na kufanikisha kuja na chupa zake za soda za kwanza za kielektroniki. Chupa hizi ni chupa ambazo zilifanikiwa kutengenezwa zikiwa ni chupa 8000 tu dunia nzima, na hii imefanya chupa hizo kuwa na bei ya hadi dollar za marekani $800 kwa chupa moja ya soda.

Advertisement

Hata hivyo, hiyo ikiwa ni bei ya chupa moja kwenye mtandao wa eBay, kwa sasa mwaka 2020 huwezi kupata chupa hizo na hata kama ukipata utaweza kuuziwa kwa pesa nyingi sio chini ya dollar hizo $800 ambayo ni sawa na takribani Tsh 1,850,000.

That’s it hiyo ndio chupa ya Coca Cola ambayo imetengenezwa kieletroniki kwa kutumia teknolojia ya OLED, kama ulivyo weza kuona chupa hii kwa sasa haipatikani na kama ukipata chupa hii jiandae kulipa zaidi ya milioni ili kumiliki chupa hii. Pia ni muhimu kujua kama Coca Cola hawato tengeneza tena chupa za namna hii, basi ni wazi kuwa baada ya miaka mitano chupa hii itaweza kuwa dili sana na pengine kuuzwa kwa mamilioni ya pesa.

Basi hadi sasa najua umejua.. Kama unataka kujua zaidi, kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kukushangaza kwenye tovuti hii. Kwa mfano, hivi unajua kampuni ya Nokia ilianza kama kiwanda cha karatasi..?. Pia unajua nchi ambazo ni maarufu kwa kutuma SMS au ujumbe mfupi..? Haya na mengine mengi yanapatikana kwenye tovuti hii unacho takiwa kufanya ni kutembelea kipengele cha Je wajua Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use