Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Chuo Kikuu Huria Chavamiwa na Wadukuzi wa Mtandao

Wadukuzi hao wa kitanzania wajitambu kwa jina la “Tanzania Hackers”
Chuo Kikuu Huria Tanzania Chuo Kikuu Huria Tanzania

Hivi karibuni wadukuzi walio jitambulisha kwa jina la “Tanzania Hackers” wamezua taharuku baina ya wafanyakazi wa chuo kikuu huria Tanzania (Open University of Tanzania) baada ya kuvamia tovuti ya mawasiliano ya chuo hicho.

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi Mmoja wa watumishi chuoni hapo ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake, alisema taharuki iliyotokea ilisababisha watumishi wa taasisi hiyo kushindwa kufanya kazi kuanzia asubuhi hadi saa 10 jioni wakati uongozi wa chuo ukiendelea na jitihada za kurejesha tovuti hiyo katika mfumo wake wa awali.

Advertisement

Gazeti la mwananchi limeandika kuwa wadukuzi hao waliacha ujumbe wa vitisho kwenye tovuti hiyo wakitaka serikali kuwapa ajira kwa mguvu au vinginevyo wangevamia hadi mifumo ya serikali.

Akizungumzia tukio hilo mkurugenzi wa Idara ya IT chuoni hapo, Dk Edephonce Nfuka alikiri kutokea kwa shambulio hilo la kimtandao huku akisikitishwa na ujumbe wa watu hao. “Tumeliona tatizo asubuhi lakini tuliweka mfumo mbadala, tunashukuru TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) nao walipoliona tatizo hilo wakatujulisha,” alisema Dk Nfuka.

Kaimu meneja mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakanjala alisema inapotokea uhalifu wa mitandao mamlaka hiyo hupokea malalamiko kutoka kwa mwathirika au polisi. aliongeza kuwa makundi yote ya kialifu mtandaoni hushulikiwa na kitengo cha “Cyber Crime Unit” ambacho kipo chini ya jeshi la polisi.

Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use