Katika hali ya kufurahisha wanafunzi wa chuo cha elimu ya biashara CBE ya Dar es salaam hivi karibuni wame furahia mara baada ya kuzinduliwa kwa internet ya bure (Free WiFi) kwenye maeneo ya chuo hicho kilichopo katika ya jiji la Dar es salaam hapa nchini Tanzania.
Katika barua iliyoandikwa na afisa uhusiano wa chuo hicho kwenda kwa wanajumuia wa chuo cha CBE ilikua ikiwataka wanafunzi wa chuo hicho kudhuria kwenye uzinduzi wa internet hiyo ya bure ambayo mkutano wake wa uzinduzi ulifanyika tarehe 30 mwezi huu 2017 huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya ilala Mh Sophia Mjema.
Katika barua hiyo afisa uhusiano huyo alidhibitisha kuwa Mradi huu ulizinduliwa rasmi kimkoa na Mhe. Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha jiji la Dar es Salaam na kufanya jiji hili kuwa bora zaidi kwa kuongeza mawasiliano kwa Wana habari, elimu kwa wanafunzi, jamii, wawekezaji na utalii. Huku ikiwa na Lengo kubwa la kujenga daraja Ia teknolojia ili kuondoa pengo kati ya wenye TEHAMA na wasio nayo, vilevile kupunguza matumizi ya karatasi, kuimarisha matumizi ya internet na ukuzaji wa elimu kwa ujumla. Barua hiyo pia ilithibitisha kuwa chuo cha elimu ya biashara CBE Dar es Salaam ndio chuo cha kwanza kunufaika na huduma za mradi huo.
Mpaka sasa bado haija julikana kuwa mradi huo utaenda wapi baada ya kutoka kwenye chuo cha CBE tawi la Dar es salaam, lakini tegemea kuona internet hiyo kwenye vyuo vingine hapa nchini Tanzania. Kama unataka kusoma barua hiyo unaweza kudownload pdf kupitia hapa.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.