Siku ya terehe 22 ya mwezi huu zilitoka taarifa ya kuwa china imezifungua huduma za kampuni ya Apple za iTunes, Movies na iBook, hii ni miezi saba tu toka huduma hizo zianze kufanya kazi katika nchi hiyo ya china, hata hivyo kampuni ya Apple ilitoa taarifa kwa Bloomberg kuwa bado inashulikia ili kurudisha huduma hizo nchini huko.
Hata hivyo jarida la New York Times la marekani lilitoa taarifa hivi karibuni kuwa china ilitoa sheria mpya ya mambo ya mitandao ambapo sheria hiyo ilianza kutumika mapema hapo wiki iliyopita ambapo ndio ilisababishwa kuzimwa kwa huduma hizo za Apple.