Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona

Roboti hizo husaidia kupunguza na kusaidia sehemu zenye virusi hivyo
China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona

Wakati virusi vya corona vikiendelea kusababisha vifo vya watu zaidi nchini China, hivi karibuni matumizi ya teknolojia yameonekana kutumika ili kupunguza maambukizi ya virusi hivyo kuendelea nchini China.

Kwa mujibu wa tovuti ya Gizmochina, China imeanza kutumia roboti za kisasa kuweza kupuliza dawa kwenye maeneo ya hospitali pamoja na kupeleka mahitaji kwenye sehemu ambazo zinasemekana kukumbwa na maambukizi hatari ya virusi hivyo vya corona.

Advertisement

Mbali na kutumika kwenye hospitali pia zipo roboti nyingine ambazo zime tengenezwa maalum kwa ajili ya kupuliza dawa kwenye mitaa mbalimbali. Inasemekana takribani roboti 140 zimesambazwa kwenye mitaa mbalimbali nchini humo, ikiwa ni kazi ya kampuni ya teknolojia ya Shanghai Dongfulong Technology Co., Ltd ambayo ndio inahusika kutengeneza na kukarabaiti roboti hizo.

China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona

Roboti nyingine zinatumika kupuliza dawa kwenye hospitali ya Wuhan Jinyintan Hospital, ikiwa pamoja na hosptali nyingine ambazo zipo karibu. Hadi siku ya leo inasemekana kuwa vifo vinavyo tokana na ugonjwa huo vimeongenezaka kutoka na kufikia watu 908, huku ikitegemewa kuwepo kwa ongezeko la idadi hiyo ya watu kutokana na kusambaa kwa ugonjwa huo.

Hata hivyo inasemekana kuwa hadi sasa idadi ya watu walioathirika na virusi hivyo nchini China imeongezeka hadi kufikia watu 40,171. Huku ikisemekana watu 28,942 wanahisiwa kuwa na virusi hivyo na idadi ya wanao ruhusiwa kutoka Hospitali baada ya kupatiwa matibabu pia imeongezeka na kufikia 2651.

China Kutumia Roboti Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya Corona

Virusi vya Corona vimeonekana kuathiri biashara mbalimbali nchini humo ikiwa pamoja na sekta mbalimbali za teknolojia, pamoja na viwanda vikubwa kama Foxconn ambacho kinatumiwa na kampuni ya Apple kutengeneza karibia asilimia 100 ya simu zake za iPhone. Kwa sasa inasemekana kuwa kampuni hiyo imepewa kibali cha kuendelea kufanya kazi ikiwa ni siku chache toka ilipo tangaza kusitisha kazi zake.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use