China Kusaidia Tanzania Kupata Wanotumia Mitandao Vibaya

Sasa wanotumia mitandao ya kijamii vibaya hapa Tanzania kubainika kwa urahisi
Mitandao ya Kijamii Vibaya Mitandao ya Kijamii Vibaya

Hivi karibuni Tanzania inaweza kuanza kuwabaini watu mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya imeripoti gazeti la nipashe, hata hivyo hatua hiyo imekuja baada ya Tanzania kutegemea kupata msaada wa mfumo mpya kutoka nchi ya Chini ili kuwezesha hilo, Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alisema watu wanaotumia lugha za matusi, kutuma picha zisizokuwa na maadili katika mitandao ya kijamii watabainika kwa urahisi kwa kutumia mfumo wa China.

Ngonyani alisema China imefanikiwa kudhibiti suala hilo kwani kitu kibaya kinapoingizwa nchini mwao kupitia mtandao, hukizuia kabla hakijaleta madhara kwa jamii. Sheria ya Makosa ya Mtandao ilipitishwa na Bunge Aprili Mosi, 2015 lakini ujio wa sheria hiyo haujaleta matokeo chanya kwa kuwa kumekuwa na matukio ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram pia. Sheria hiyo ambayo tayari imeshaanza kutekelezwa ilipelekwa bungeni kwa hati ya dharura Ngonyani.

Advertisement

Ngonyani aliyekuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vyombo vya habari na matumizi ya mtandao uliofanyika jijini Dar es Salaam, alisema kuna idadi kubwa ya wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii. “Lakini baadhi yao huitumia kwa kuwatukana watu na hata kuweka vitu visivyotakiwa kwa maadili ya Kitanzania,” aliendelea kusema “Kama mtu amekutumia ujumbe mbaya, tunataka tuwe na uwezo wa kumkamata na kumchukulia hatua.

Kwa mujibu wa gazeti la nipashe Ngoyani aliendelea kusema “(mtu) amekutumia barua pepe, au ametuma picha mbaya kwenye WhatsApp, wenzetu China wameweza kuwanasa kwa urahisi “Sasa na sisi tunataka kujifunza hilo ili tuanze kuwabaini.” Mhandisi Ngonyani alisema serikali inaandaa mfumo huo wa kuwabaini moja kwa moja watumiaji wabaya wa mitandao na kwamba pindi utakapokamilika utapelekwa katika Baraza la Mawaziri; kisha kupelekwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria.

“Mfumo huo ukikamilika tutaweza kujua ujumbe huu umetoka kwa nani, kwa sababu kwa sasa hivi mtu anaweza kutumia simu ya mtu mwingine kutuma ujumbe mbaya,” alisema zaidi. “Sasa ni lazima tutafute teknolojia mpya ambayo hata mtu akitumia simu (namba) ya mtu na kuitumia vibaya tunamkamata. Kiongozi huyo pia alisema kwa sasa serikali imefikia hatua nzuri ya udhibiti wa wezi wa fedha wa mitandao lakini bado inatatizwa na mitandao ya kijamii kutoka nje ya nchi kama vile WhatsApp, Facebook na Instagram.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Nipashe Ipp Media

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use