China yaazimia kuanzisha mfuko wa jamii unaoendeshwa na serikali ambao utasaidia na kuunga mkono juhudi za nchi hiyo katika kuzalisha chipset za kielektroniki kwa ajili ya simu na vifaa vingine vya kielektroniki.
Mfuko huo unatazamiwa kukusanya takribani Dola za Kimarekani Bilioni 40 (Shilingi za Kitanzania Trilioni 100.2) ili kuwekeza katika makampuni yanayofanya utafiti na uzalishaji wa chipset hizo nchini humo.
Tangu Marekani ilipoweka vikwazo kwa nchi ya China, hasa katika eneo la kiteknolojia, China imechochea kasi yake ya kuboresha teknolojia yao binafsi ili kuweza kujitegemea katika mifumo yao na vifaa vyao vingi, ikiwa wazi kwamba sehemu kubwa tu ya teknolojia ambazo baadhi ya makampuni ya kichina ilikuwa ni kutokea nchi kama Marekani.
Teknolojia kama za ubunifu na uzalishaji wa chipset zilizotokea Marekani zimewekewa vizuizi kutumika nchini China, na Serikali ya China kwa kutaka kuwa mbele katika mbio za kiteknolojia imeamua kuwekeza nguvu zake zaidi katika kuboresha teknolojia yake ya ndani kwa kuyapa mguvu na kuyaunga mkono mashirika na makampuni ya kiteknolojia ya ndani.
Huu hautakuwa mfuko wa kwanza ambao umeunda nchini humo, ila takribani wa tatu, mingine ikiwa imeundwa mwaka 2014 na 2019. Itabaki kutazamwa ndani ya miaka kadhaa mbele, nafasi ya nchi ya Chinakatika maendeleo ya kiteknolojia itakuwa katika uimara upi, ikiwa tayari mojawapo ya nchi zenye ukuaji wa kasi sana katika teknolojia.