Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Channel Zenye Subscriber Wengi Zaidi Hadi Sasa (2019)

Hizi ndio channel maarufu duniani kupitia mtandao wa YouTube
Hizi Hapa Channel Zenye Subscriber Wengi Zaidi Hadi Sasa (2019) Hizi Hapa Channel Zenye Subscriber Wengi Zaidi Hadi Sasa (2019)

Mtandao wa YouTube ulizaliwa takribani miaka 14 iliyopita na kwa kipindi chote hicho hadi sasa zipo baadhi ya channel ambazo zinafanya vizuri sana hadi kufanikiwa kuvunja rekodi ambayo ukweli ni kitu cha kupongezwa sana.

Kwa bahati mbaya hadi sasa hakuna channel yoyote ambayo inaongoza kwa kuwa na subscriber wengi zaidi duniani ambayo inatoka nchi za Afrika hivyo usitegemee utaweza kuona jina lolote la channel kutoka Afrika kwenye list hii. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie List hii.

Advertisement

10. Canal KonZilla – Subscriber Milioni 51

Konrad Dantas, anayejulikana zaidi kwa jina la KondZilla, au KOND, ni mwandishi wa skrini wa Brazil na mtayarishaji muongozaji. Yeye ndiye mwanzilishi wa KondZilla Record, ambayo ni kampuni ya utengenezaji wa video za muziki na lebo ya rekodi, mara nyingi hupewa sifa ya kuwa mtu maarufu wa muziki wa funk ostentação.

9. Set India – Subscriber Milioni 54

Hii ni channel ya kulipia ya Sony Entertainment Television ya nchini India channel hii imekuwa maarufu sana kupitia mtandao wa YouTube kutokana na kuweka filamu na series nyingi nzuri sana za india ambazo huangaliwa na watu wengi hata hapa Afrika.

8. Cocomelon – Nursery Rhymes – Subscriber Milioni 58

Kama wewe ni mpenzi wa katuni kwa ajili ya watoto basi lazima utakuwa unajua channel hii, channel hii ni moja kati ya channel maarufu zaidi kwa kuweka na kutengeneza video za katuni kwa ajili ya watoto kujifunza vitu mbalimbali.

7. 5-Minute Crafts – Subscriber Milioni 60

Kama umekwepo kwenye mtandao wa YouTube au Instagram kwa muda mrefu basi lazima unaijua channel hii, Kupitia channel hiyo utaweza kujifunza maujanja mbalimbali ya maisha kwa kutumia vitu mbalimbali vinavyo tuzunguka.

6. YouTube Sports – Subscriber Milioni 75

YouTube Sport ni channel ambayo kama wewe ni mpenzi wa michezo basi niakushauri fanya kusabscribe sasa hivi. Channel hii tofauti na channel nyingine hii inatengenezwa na YouTube na inakusanya video mbalimbali za matukio muhimu pamoja na habari za michezo, haijalishi kutoka wapi channel hii inaleta michezo yote mezani.

5. YouTube Gaming – Subscriber Milioni 83

Kama wewe ni mpenzi wa Game basi YouTube Gaming ni channel ambayo imetengenezwa na YouTube kwaajili yako. Channel hii inahusisha video za live kutoka channel mbalimbali ambazo zinaonyesha watu wakicheza game mbalimbali kupitia vifaa vya ina tofauti.

4. YouTube Movies – Subscriber Milioni 87

Kama unapenda filamu basi channel ya YouTube movie ni kwaajili yako, channel hii ni maarufu kwa kuweka filamu mbalimbali pamoja na trailer kutoka kwenye channel za watu mbalimbali kupitia mtandao wa YouTube, kama video yako ni filamu na imeangaliwa na watu wengi basi usishangae ikawekwa kwenye channel hii ya YouTube Movies. Kwa Tanzania channel hii huwezi kuona video zake.

3. PewDiePie – Subscriber Milioni 100

Kama upo kwenye mtandao wa Youtube kwa muda mrefu basi lazima unamjua huyu jamaa, inasemekana kuwa yeye ni mmoja wa watu wanaongoza kwa kupata pesa nyingi kutoka na mtandao wa YouTube. Inasemekana kuwa jamaa huyo amepata mafanikio makubwa kupitia mtandao huo kiasi kwamba ndio kazi pekee anayo ifanya.

2. YouTube Music – Subscriber Milioni 107

YouTube Music ni channel ambayo inachanganya video mbalimbali za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali. Channel hiyo imetengenezwa na YouTube na inachukua video kutoka kwa wasanii wote maarufu kupitia mtandao wa YouTube.

1. Channel Yenye Subscriber Wengi Zaidi

T-Series ndio jina la channel yenye Subscriber wengi kuliko channel zote kupitia mtandao wa YouTube, hadi sasa channel hiyo ndio inaongoza kwa kuwa na Subscriber wengi zaidi Duniani ina jumla ya Subscriber Milioni 109. Channel hii ni channel inayoweka video za muziki kutoka nchini India.

Na hizo ndio channel 10 zenye subscriber wengi zaid kupitia mtandao wa YouTube, zipo channel nyingi bora lakini hizi hapa ndio channel bora zaidi kupitia mtandao wa YouTube. Kama unataka kujua channel maarufu zaidi kwa hapa Tanzania kwa mwaka jana 2018 basi unaweza kusoma hapa. Kwa habari zaidi usisahau kusubscribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani kuna kitu kikubwa kinakuja.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use