Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Kuleta Aina Mpya ya Channel kwa Ajili ya Wanamuziki

Habari Njema kwa Wanamuziki Wanaotumia Mtandao wa YouTube
Channel mpya YouTube Channel mpya YouTube

Ni kweli kuwa wanamuziki wengi sasa hutegemea mtandao wa Youtube kutoa video au miziki mbalimbali, lakini kutokana na watumiaji wa mtandao huo kuwa wengi ni vigumu sana kupata channel halisi ya msanii unaye mtafuta, sasa YouTube imekuja na njia mpya ya kuhakikisha unapata channel halisi ya msanii unaye mtafuta.

Hivi karibuni YouTube imetangaza kuja na aina mpya ya channel ambazo hizi zitakuwa ni kwa ajili ya wasanii wa muziki pekee, channel hizi zitakuwa na utofauti kidogo kwani itakuwa ni muungano wa channel zote za msanii na kuweza kutengeneza akaunti moja ambayo itawekewa alama maalum ambayo itawakilisha kuwa hiyo ndio channel halisi ya msanii unaye mtafuta.

Advertisement

Channel hiyo moja itaunganisha channel zote za mwanamuziki za msanii unayemtaka yani, kwa mfano kama msanii ana channel ya Youtube ya kawaida na anayo channel ya Youtube ya Vevo basi channel zote mbili zitaunganishwa na kutengeneza channel moja ambayo itawekewa alama maalum kuonyesha hiyo ndio channel halisi ya mwanamuziki.

Youtube imesema mfumo huu mpya utasaidia watumiaji wa mtandao huo kuweza kupata channel halisi ya msanii pamoja na kuweza kujiunga na msanii kwenye akaunti moja kuliko kujiunga na channel mbili tofauti.

Sehemu hii inatarajiwa kuja siku za karibuni na alama ya ” Official Artist Channel YouTube Kuleta Aina Mpya ya Channel kwa Ajili ya Wanamuziki” itakuwa inaonekana kwenye kurasa zote za mtandao wa Youtube ikiwa pamoja na kwenye ukurasa maalum wa kutafuta au search page. Kwa habari zaidi unaweza kusoma ukurasa maalum wa YouTube kupitia Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use