Maisha yamebadilika na ukweli simu zetu za siku hizi zinaonekana kupunguwa uweza wa kudumu na chaji kadri siku zinavyo kwenda, kusuluhisha hilo kampuni moja ya teknolojia imetengeneza kalamu yenye uwezo wa kuchaji simu yako.
Kalamu hiyo iliyopewa jina la Charge Write ni kalamu ya kwanza duniani kuwa na uwezo wa kuchaji simu, kutumika kama hard disk pamoja na kutumika kama kifutio cha kioo cha simu yako. Kalamu hiyo imetengenezwa pamoja na kubuniwa na wataalam Shaun Teblum pamoja na Rob Gold.
Ili kuchaji kalamu hiyo utachomeka kalamu hiyo kwenye sehemu yoyote yenye USB kisha kalamu hiyo itaonyesha inaingia chaji moja kwa moja kwa kuwasha taa ya rangi ya blue, kalamu hiyo inapatikana kwa aina mbili za Charge Write pamoja na Charge Write Plus zikiwa na gharama ya dollar $29 na dollar $39 kwa Charge Write Plus sawa na shilingi za kitanzania tsh 90,000 kwa Charger Write Plus na shilingi 65,000 kwa Charge Write.
Kwa habari zaidi za teknolojia download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kuwa wa kwanza kupta habari zote za teknolojia, pia unaweza kuungana na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube ili kuapata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.