Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19

Chaja hii ina uwezo wa kuchaji battery ya 4000mAh kwa dakika 19
Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19 Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19

Kwa sasa simu nyingi zinakuja na teknolojia ya fast charging, teknolojia hii inawezesha simu kuweza kupokea chaji kwa haraka zaidi na hivyo kufanya battery ya simu husika kujaa kwa haraka.

Ukweli ni kwamba, japokuwa teknolojia hii inapatikana kwenye simu nyingi lakini ni wazi kuwa kuna wakati bado unaona kama kusubiri simu iweze kujaa chaji hadi asilimia 100 ndani ya nusu saa bado unaona kama ni muda mrefu.

Advertisement

Kuliona hili kampuni ya Xiaomi hivi karibuni imetambulisha chaja mpya kabisa ambayo inayo uwezo wa kujaza simu hadi asilimia 100 ndani ya dakika 19 tu. Chaji hiyo ina uwezo wa kuchaji simu husika kuanzia asilimia 0 hadi kufikia asilimia 100 ndani ya dakika hizo 19.

Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, chaja yenye ambayo ni chaja ya mfumo wa wireless fast charging yenye Walt 80W, ina uwezo wa kuchaji simu ya Xiaomi Mi 10 Pro kwa muda usiozidi dakika hizo 19.

Miaka ya nyuma kampuni ya Samsung iligundua teknolojia ya kuchaji battery ya simu kwa dakika 12, lakini teknolojia hiyo hadi sasa haijaweza kuonekana kama ilivyo teknolojia hii ya kampuni ya Xiaomi. Hadi sasa zipo chaja zenye uwezo mkubwa wa kuchaji simu kwa haraka kama vile chaji yenye Walt 55W ambayo pia ni chaja kutoka Xiaomi, chaja ya Huawei yenye Walt 40W, pamoja na chaja ya Oppo yenye Walt 125W yenye uwezo wa kuchaji battery ya simu kwa DK 20.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use