Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ushindani Mkali TECNO CAMON 18 Premier Vs Galaxy A52

TECNO CAMON 18 Premier inapatikana kwa TZS 790,000
Ushindani Mkali TECNO CAMON 18 Premier Vs Galaxy A52 Ushindani Mkali TECNO CAMON 18 Premier Vs Galaxy A52

Kampuni ya simu za mkononi TECNO inatarajia kuachia toleo jipya ya simu janja TECNO CAMON 18 hivi karibuni ambayo italeta ushindani mkubwa na simu kutoka kampuni ya Samsung. CAMON 18 Premier ina sifa kuizidi simu ya Samsung Galaxy A52.

Ushindani Mkali TECNO CAMON 18 Premier Vs Galaxy A52

Advertisement

Kamera

TECNO CAMON 18 Premier ina sifa ya kipekee kuwa na GIMBAL CAMERA, ambayo itamsaidia kuchukua video kali na thabiti bila kutikisika., tofauti na simu ya Samsung Galaxy A52 ambayo haina sifa hiyo.

Betri na Uwezo wa Kuchaji

Kwa upande wa kuchaji simu TECNO CAMON 18 Premier imeongoza ambayo ina betri ya 4750mAh inaweza kujaa chaji kwa haraka kutokana na kuwa simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 33 W.

Tofauti na Samsung Galaxy A52 simu hii inakuja na battery ya 4700 mAh, ambayo ina 25W

Kioo

Tukianzia kwenye upande wa kioo au display, TECNO CAMON 18 Premier pia inaongoza inakuja na kioo cha inch 6.7 tofauti na simu ya Galaxy A52 yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.5.

Mbali na hayo simu ya TECNO CAMON 18 Premier ina kioo cha AMOLED chenye refresh rate ya 120Hz kubwa zaidi ya Samsung Galaxy A52.

Storage (ROM)

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, TECNO CAMON 18 Premier inakuja uhifadhi wa 256GB, tofauti na Samsung Galaxy A52 ina uhifadhi wa 128GB.

Ushindani Mkali TECNO CAMON 18 Premier Vs Galaxy A52

RAM

Kwa upande wa RAM ni wazi kuwa simu hizi zinalingana zote zikiwa na RAM ya GB 8, hapa lakini kwa upande wa TECNO CAMON 18 Premier unapata toleo lenye GB 8 za RAM huku kwa Samsung Galaxy A52 ukiwa unapata matoleo ya GB 4, 6 na 8.

Bei na Upatikanaji

Mpaka sasa tetesi zinasema TECNO CAMON 18 Premier itapatikana kuanzia Tsh 790,000/= ambayo ni bei rahisi sana ukilinganisha na sifa ambazo simu hiyo ipo nayo. Tofauti na simu ya Samsung Galaxy A52 ambayo inapatikana kwa Tsh 1,000,000/=.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use