Kama wewe ni mpenzi wa Game ni wazi kuwa umepita muda mrefu sana toka tuongelee maswala haya, lakini kwa sababu huu ni mwaka mpya nakuahidi tuendelea kuja na makala nyingi sana kwa ajili yako wewe mpenzi wa Games.
Sasa baada ya kusema hayo, leo nina taarifa njema kwako kwani wapenzi wa Game za Action wataenda kufurahia game ya Call of Duty kupitia simu za mkononi za Android na iOS.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kampuni ya Activision kwa kushirikiana na kampuni ya Tencent imetangaza kuwa Game hiyo ya Call of Duty inakuja kwenye simu za mkononi za Android na iOS huku ikiwa na uwezo wa kuruhusu watu zaidi ya wawili kucheza game hiyo. Kama wewe ni mpenzi wa game kama PUBG au Fortnite basi game hii ni nyingine ya kuongeza kwenye list yako.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti mbalimbali, Game hii mpya inatarajiwa kutoka mapema mwaka huu, lakini pia inatarajiwa kutoka kwanza kwenye Play Store. Unaweza kujisajili ili kupata taarifa game hii itakapotoka kupitia masoko ya Play Store. Unaweza kufanya hivyo kwa kubofya link hapo chini.
Lakini pia kwa sababu hapa ni Tanzania Tech, basi unaweza kujaribu Game hii kwa kutumia maujanja haya ambayo ninaenda kuonyesha hapa. Kitu cha muhimu kujua ni kuwa maujanja haya yana wezekana kwa kutumia simu ya Android pekee kwa sasa.
Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye tovuti hii HAPA, kisha download file la APK lenye MB 66.5 kisha install kwenye simu yako. Kumbuka baada ya kuinstall usiwashe programu hiyo kwanza badala yake endelea kwenye hatua zinazofuata.
Hatua ya pili download OBB file hili ni kubwa kidogo lina GB 1.06, folder hili lipo kwenye mfumo wa ZIP hivyo download programu ya ku-unzip kama simu yako haina uwezo wa kufungua file hilo. Baada ya hapo Copy kila kitu kilichopo ndani ya Folder hilo kisha tafuta Folder la Call of Duty OBB na weka vitu vyote humo.
Baada ya hapa washa Game yenyewe na utaweza kuanza kucheza game hiyo moja kwa moja. Kumbuka unaweza kukutana na matatizo ya Game kunata nata au ku-stack ikiwa na matatizo mengine, hii inasababishwa na kuwa game hii bado iko kwenye hatua za awali. Kama unataka habari nyingine za Games unaweza kusoma hapa.