Brela Kuanza Usajili wa Makampuni Mtandaoni Kuanzia Feb 1

Sasa watanzania wataweza kuanza kusajili makampuni kupitia mtandao
Brela Tanzania Brela Tanzania

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), hivi karibuni ilitangaza kuwa ina-andaa mfumo mpya ambao utawezesha watanzania kusajili kampuni kupitia mtandao, hivi leo BRELA imatangaza sasa mfumo huo umekamilika na utanza kufanya kazi rasmi kuanzia Feb 1 mwaka huu 2018.

Kwa mujibu wa tangazo lililo tolewa na BRELA, Mfumo huo utamwezesha Mteja kupata huduma popote pale alipo bila kwenda kwenye ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni na bila kuitaji ujuzi mkubwa sana. Hata hivyo BRELA imeainisha kuwa mteja ataitaji Kuwa na Namba ya Utambulisho wa utaifa (National Identification Number (NIN) inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Advertisement

Tangazo hilo pia limeeleza kuwa, kama anaye sajili kampuni anatarajia kuwa Mkurugenzi wa kampuni (Director) basi ni lazima awe tayari na Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) inayotolewa na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA).

Vilevile BRELA imeainisha kuwa anaetaka kusajili kampuni ni lazima wakati anaandaa Malengo na katiba ya kampuni (Memorandum and Article of Association) ahakikishe malengo unayo jiwekea yameendana na shughuli unazo zichagua kwenye mfumo wa ORS kwa mujibu wa ‘ISIC classication’ ambayo itapatikana kwenye mfumo huo na kwenye Tovuti ya BRELA.

Hapo mwanzo BRELA ilikuwa inatoa huduma za kusajili majina ya biashara pekee kupitia mtandao lakini sasa hata usajili wa makampuni pia utakuwa kupitia kwenye mtandao, kama unataka kujua zaidi unaweza kutembelea tovuti ya BRELA au unaweza kusoma notice ya tangazo hilo HAPA.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

6 comments
  1. nataka jinsi kusajili jina la kampuni nielekezeni
    nina majina matatu
    1. SKD INVESTMENT CO .TZ LTD

    2.KDS INVESTMENTCO LTD

    3. SGKD COMPANY LTD

  2. Nimesahau kuandika jina hapo juu nikitaka kusajili mojawapo kati ya majina matatu ambayo ni
    1.SKD INVESTMENT LTD
    2.KDS INVESTMENT LTD
    3. SGKD COMPANY LTD
    Nisaidie nifanyeje

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use