Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Boomplay Kushirikiana Kibiashara na Warner Music Group

Boomplay kusambaza kazi za muziki zaidi ya milioni 1 kutoka Warner Music
Boomplay Kushirikiana Kibiashara na Warner Music Group Boomplay Kushirikiana Kibiashara na Warner Music Group

Kama wengi wetu tunavyo jua, Boomplay ni app inayotoa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, sasa hivi karibuni boomplay imesaini makubaliano ya kushirikiana kibiashara na Warner Music kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa kazi za muziki wa kampuni hiyo maeneo mengi zaidi duniani.

Moja kati ya makubaliano hayo ni pamoja na kuipa fursa Boomplay, kusambaza kazi za muziki zaidi ya milioni moja kutoka Warner Music kwenda kwa watumiaji wake nchini Tanzania na mataifa mengine tisa ya kiafrika ikiwemo Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Kenya, Nigeria, Rwanda, Senegal, Uganda na Zambia.

Advertisement

Ushirikiano huu pia utawawezesha wasanii wa Warner Music kujitangaza zaidi na tena kwa haraka mbele ya mamilioni ya watumiaji wa Boomplay na kuiwezesha app hiyo ya kijanja kuifikia dhamira yake ya kukusanya kazi za muziki kutoka sehemu mbali mbali za dunia na kuzileta barani Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Boomplay, Bwana Joe He, amesema, “Makubaliano haya na makampuni makubwa ya muziki ya kimataifa kama Warner Music, yanatuwezesha sisi kuyakaribia mafanikio ya malengo yetu ya kujenga jukwaa kubwa la muziki linaloaminika na wengi barani Afrika”

“Tunataka kila mpenda muziki awe na uwezo wa kupata nyimbo na video, wakati wowote na mahali popote. Tunatarajia uwepo wa mafanikio bora kupitia ushirikiano huu na muendelezo mzuri wa kibiasha tukiwa na Warner Music hasa katika kipindi hiki kizuri kwenye fani ya muziki Afrika” aliongeza Bwana He.

Pia, Meneja wa Boomplay Tanzania, Bi Natasha Stambuli amesema, “Tunatarajia mafanikio makubwa na fursa mbalimbali yakiwa ni matokeo ya makubaliano kama haya katika tasnia ya muziki nchini Tanzania. Huu ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi hapo mbeleni kwa Boomplay pamoja na Warner Music.”

Naye Alfonso Perez Soto, ambaye ni Makamu wa rais wa Warner Music huko Ulaya Mashariki, Mashariki ya Kati na Afrika amebainisha kwamba “Tuna furaha kushirikiana na Boomplay kuleta kazi kutoka kwa wasanii wetu kwa mamilioni ya wasikiliza na wapenzi wa muziki barani Afrika. Boomplay tayari imewafikia watu wengi barani Afrika huku wakiendelea kupanua wigo. Hii ni fursa kubwa kwa wasanii wetu kupata mashabiki wengi zaidi.”

“Ningependa kuwashukuru, Charlie White, Marc Latilla na Reni Adadevoh kutoka Warner Music kwa mchango wao mkubwa kusaidia kufanikisha makubaliano haya” aliongeza Bwana Soto.

Toka mwaka uliopita, Boomplay imeendelea kutikisa anga la muziki kwa kutangaza ushirikiano na makampuni mbali mbali makubwa ili kupata watumiaji wengi zaidi kila mwezi na kutoa version (toleo) ya iOS mwezi Disemba mwaka 2018.

Pamoja na uwepo wa lebo kubwa za muziki zinazojiunga na Boomplay, app hii imejidhatiti kwa kujenga na kuboresha nafasi yake barani Afrika. Boomplay, ambayo mpaka kufikia mwezi Februari, 2019, ilijikusanyia zaidi ya watumiaji milioni 42, ina kazi za muziki zaidi ya nyimbo milioni 5, na maelfu ya video kutoka kwa wasanii wa Tanzania na wa kimataifa.

Kuhusu Boomplay

Boomplay (ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama Boomplayer), ni jukwaa linalotoa huduma ya kusikiliza na kupakua (download) muziki ambayo ipo chini ya umiliki wa kampuni ya Transsnet Music Limited.

Malengo ya app hii ni kutengeneza jukwaa kubwa na la kutegemewa na wasanii na wazalishaji wa muziki katika usambazaji wa kazi hizo za sanaa. Boomplay ilishinda tuzo ya “Application bora Africa” kwenye tuzo za “AppsAfrica Awards” mwaka 2017.

Kwa sasa Boomplay ndio application kubwa na inayokuwa kwa kasi sana barani Afrika, ikiwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5.

Watumiaji wake wanaweza kusikiliza na kuangalia video bure, kwa kujisajili (subscribe) kupitia vifurushi vya siku,wiki au vile vya mwezi ambapo ambavyo vinawawezesha kuhifadhi (save) nyimbo offline au kununua nyimbo. Huduma hiyo kwa sasa inapatikana Android, iOS na wavuti. Unaweza kudownload app ya Boomplay hapo chini.

Boomplay – Android

Boomplay – iOS

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use