Hivi karibuni wizara ya afya imetengaza njia mpya ya kuweza kuhifadhi nafasi au kufanya booking ya kupata chanjo ya Uviko 19 au Covid-19 kupitia mtandao.
Njia hii ni rahisi na itasaidia watu wengi kuweza kuhifadhi nafasi au kufanya booking ya kupata chanjo kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa afya hapa Tanzania.
Mahitaji ya Booking Mtandaoni Chanjo ya Uviko-19
Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa na kitambulisho kitakacho kutambulisha, kwa mujibu wa tovuti hiyo vifuatavyo ni vitambulisho vinavyo kubaliwa kwenye mfumo huo.
- Kitambulisho cha Taifa NIDA
- (Voters ID) Kitambulisho cha Kupiga Kura
- Pass ya Kusafiria (Passports)
- Leseni ya Udereva (Drivers License Number)
Baada ya kuwa na kitambulisho kimoja kati ya hivyo moja kwa moja unaweza kutembelea tovuti maalum ya wizara ya afya kupitia link hapo chini. Hakikisha unafuata hatua zote moja baada ya nyingine ili kuweza kukamilisha kwa usahihi kufanya booking ya chanjo hiyo ya uviko 19.
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea tovuti ya wizara ya afya hapo chini, pia unaweza kuwasiliana na wizara hiyo kwa taarifa zaidi.
Simu: +255 24 2231614
Nukushi: +255 24 2231613
Barua pepe: info@mohz.go.tz
Tovuti: www.mohz.go.tz