Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Miliki Tovuti ya Blogger ya Kupakua Nyimbo Mpya Bure

Utaweza kutengeneza pesa kupitia tovuti ya blogger ya kupakua nyimbo mpya
Miliki Tovuti ya Blogger ya Kupakua Nyimbo Mpya Bure Miliki Tovuti ya Blogger ya Kupakua Nyimbo Mpya Bure

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa mtandao wa blogger basi pengine huu ni wakati wako wa kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia njia mbalimbali ambazo tunaendelea kuzionyesha hapa Tanzania tech.

Kwa siku ya leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kutengeneza tovuti ya blogger ambayo itakuwa inasaidia watu mbalimbali kudownload nyimbo za mp3 kutoka mtandao wa youtube. Uzuri wa tovuti hii inaweza kukusaidia kutengeneza pesa mtandao kupitia mtandao wa Adsense kwa urahisi na haraka.

Advertisement

Miliki Tovuti ya Blogger ya Kupakua Nyimbo Mpya Bure

Kabla ya kuendelea ni muhimu kujua kuwa tovuti hii imetengenezwa kwa blogger na unaweza kutengeneza ya kwako pia kama utafuata hatua zote ambazo nitakuelekeza kupitia makala hii. Basi bila kupoteza muda moja kwa moja unaweza kuangalia mfano hapo chini.

Angalia Mfano Hapa

Baada ya kuangalia mfano na kuona kama ni kitu unacho hitaji basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye hatua za jinsi ya kutengeneza tovuti hii.

Kwa kuanza download templent ya tovuti hii kisha hakikisha unafuata hatua kwa hatua kama ninavyo onyesha hapo chini. Bila kufanya hivyo tovuti hiyo haitoweza kufanya kazi.

Download Hapa

Kwa kuanza ingia kwenye blogger.com, kisha tengeneza blog mpya moja kwa moja. Kama ujui jinsi ya kutengeneza blog kupitia blogger unaweza kuangalia hapa hatua kwa hatua jinsi ya kufanya.

Baada ya kutengeneza blog yako moja kwa moja bofya sehemu ya Theme.

Miliki Tovuti ya Blogger ya Kupakua Nyimbo Mpya Bure

Baada ya hapo, bofya kwenye sehemu ya mshale wa chini pembeni ya kitufe cha Customize kinacho onekana kwenye ukurasa huo wa Theme.

Kama unavyoweza kuona kwenye video fupi hapo juu, bofya sehemu ya mshale kama inavyonekana kisha bofya sehemu ya Switch to first generation Classic theme kisha baada ya hapo bofya sehemu ya Switch without a Backup.

Baada ya hapo bofya sehemu ya edit html kisha fungua file ulilo download awali pale juu au bofya hapo chini kuweza kucopy code kama unatumia simu kisha paste kwenye sehemu hiyo ya blogger.

Bofya Ku-copy File kwa Simu

Baada ya kucopy moja kwa moja save file hilo kwa kubofya sehemu ya kusave kwenye blogger na moja kwa moja tembelea tovuti yako utaweza kuona tayari umeweza kupata tovuti yako yenye uwezo wa kudownload video kuwa mp3.

Ili kutumia tovuti hiyo unatakiwa ku-copy link ya video kutoka kwenye mtandao wa YouTube, kisha moja kwa moja paste kwenye tovuti hiyo kwenye sehemu ya Download, subiri kidogo kisha utaweza kuona sehemu ya kudownload kwa chini yake.

Hadi hapo utakuwa umemaliza, unaweza kuweka custom domain kwenye tovuti yako kisha moja kwa moja omba matangazo kupitia adsense na utaweza kuanza kutengeneza pesa moja kwa moja.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use